Facebook

Tuesday 13 January 2015

Hivi ndivyo Kura za Ballon d’Or zilipigwa hadi washindi kupatikana.

IMG_0818.JPG
Hapo jana usiku zimefanyika tuzo za Ballon d’Or ambapo wachezaji wa mwaka uliopita walikuwa wakitunukiwa na shirikisho la soka ulimwenguni FiFA.

Mwanasoka bora wa msimu uliopita mreno Cristiano Ronaldo ameibuka mshindi kwa mara ya pili mfululizo.

Ronaldo alikuwa akichuana na Lionel Messi na Manuel Neur katika tuzo hizo.
Lakini baada ya kusubiri kwa takribani miezi miwili hatimaye nahodha huyo wa Ureno akatangazwa kushinda tuzo hiyo – ikiwa sasa ni mara ya 3.

Cristiano Ronaldo alipata asilimia 37.66 ya kura zote huku Lionel Messi (15.76%) na Manuel_Neuer (15.72%).
Katika vipengele vingine – James Rodriguez alishinda tuzo ya goli bora la mwaka, huku Nedine Kassler akishinda tuzo ya mwanasoka bora mwanamke.

Manuel Neur alishinda tuzo ya golikipa bora huku kocha wake Joachim Law wa Ujerumani akishinda tuzo ya kocha bora.

0 comments:

Post a Comment