Facebook

Saturday 31 January 2015

Wema sepetu akamatwa na polisi kwa bajaji


 
 
Mwana dada muigizaji wa filamu za kitanzania asie kauka kwenye vichwa vya habari kwenye mitandao na midomoni mwa watu,amefanya tukio jingine la kushangaza jamii kitendo kilicho pelekea mapolisi kuja kumkamata.
Polisi wamejikuta wanapata heka heka ya kumshika mwana dada Wema Sepetu kwa kosa la kupiga muziki kwa sauti kubwa usiku kucha bila kibali hali iliyo pelekea kuwaudhi jirani zake.
Polisi hao walifika asubuhi ya leo kwa lengo la kumkamata mwana dada huyo asiye ishiwa vimbwanga kila siku,ndipo Wema alipo anzisha vurugu.
 
Wema yeye anavyo dai ni kwamba kulikua na birthday ya rafiki yake aliefahamika kwa jina moja Neema,mmoja wa majirani wa Wema alisema kwamba hua ndio tabia yake ya kufanya sherehe na kufungulia muziki kwa sauti kubwa zaidi kitu ambacho kinasababisha kero kwa majirani zake.
Polisi waliamua kuchukua spika za redio hiyo na kumbeba Neema alie semekana ndie aliyekuwa mwenye sherehe.

0 comments:

Post a Comment