Facebook

Saturday 17 January 2015

Cameroon kupambana na Boko Haram

 
Serikali ya Cameroon imesema Chad itatuma kikosi kikubwa cha wanajeshi wake kupambana na wapiganaji wa kiisilamu wa Boko Haram mpakani mwa Nigeria na nchi hio.
Tangazo hili limetolewa siku moja baada ya Chad kusema kwamba itaunga mkono jirani yake Nigeria katika harakati dhidi ya wapiganaji wa kiisilamu wa Boko Haram.

Hakuna taarifa zozote zimetolewa kuhusu idadi kamili ya wanajeshi watakaopelekwa huko au siku.
Mnamo siku ya Jumanne, Cameroon ilisema kwamba iliwaua wapiganaji 143 wa Boko Haram, ambao walishambulia kambi zake katika eneo la Kolofata karibu na mpaka na Nigeria.
Ilisema kuwa mwanajeshi mmoja alifariki wakati wa mashambulizi hayo ambayo yalisababisha ufyatulianaji risasi mkali kati ya wanajeshi na waasi hao kwa muda wa saa tano.

lilikuwa shambulizi la kwanza kubwa kufanywa na Boko Haram dhidi ya Cameroon tangu kundi hilo kutishia kiongozi wa nchi hio katika kanda ya video waliyoiweka kwenye mtandao mapema mwezi huu.
Wanamgambo hao wameteka miji na vijiji kadhaa ambavyo wanavidhibiti Kaskazini Mashariki mwa Nigeria katika harakati zao ambazo wameziendeleza kwa miaka sita sasa.

0 comments:

Post a Comment