Facebook

Sunday 25 January 2015

Chelsea,Man city,Southampton na Totenham nje kombe la F.A

 

Vilevile kilabu ya daraja la kwanza Bradford City ilionyesha mchezo wa hali ya juu ilipotoka nyuma 2-0 na kuweza kuwashinda viongozi wa ligi ya Uingereza Chelsea 4-2 katika mechi ya FA ilioijaa mbwembwe za aina aina.
Katika uwanja wa Totenham bao la Jeffrey Schlupp lilisaidia Leicester kuishinda Totenham.
Leicester ilikuwa nyuma kwa bao moja kabla ya kusawazisha na kuongeza la ushindi.

 Uwanjani Southampton Mshambuliaji Marouane Chamakh alifunga mabao mawili na kuisaidia kilabu ya Crystal palace kupata ushindi wa 3-2 dhidi ya Southampton katika mechi iliokuwa na mchezo mzuri.

Matokeo ya FA
Cardiff 1 - 2 Reading FT
Chelsea 2 - 4 Bradford FT
Derby 2 - 0 Chesterfield FT
Man City 0 - 2 Middlesbrough FT
Preston 1 - 1 Sheff Utd FT
Southampton 2 - 3 Crystal Palace FT
Sunderland 0 - 0 Fulham FT
Tottenham 1 - 2 Leicester FT

0 comments:

Post a Comment