Mwanablogu Raif Badawi ana majeraha ambayo hayawezi kumruhusu kupewa adhabu nyingine
SaudiArabia imeahirisha adhabu ya kumchapa viboko mwanablogu Raif Badawi kwa sababu ya afya yake.
Mwanablogu huyo ambaye pia ni mwanaharakati aliyeanzisha mtandao wa 'Forum Liberal Saudi Network' ambao sasa umefungwa na serikali, alitarajiwa kuchapwa viboko 50 hadharani baada ya sala ya Ijumaa hii leo.
Mwezi Mei mwaka jana, alihukumiwa miaka 10 jela na kuandikiwa adhabu ya mijeledi 1,000 kwa kuitusi dini ya kiisilamu pamoja na kutoitii sheria.
Bwana Badawi
alipokea awamu ya kwanza ya viboko Ijumaa iliyopita huku kesi yake
ikisababisha tuhuma kutoka kwa jamii ya kimataifa dhidi ya Serikali ya
Saudia. Hata hivyo serikali haikutoa tamko lolote kwa kukosolewa.
Kadhalika serikali hio ingali kutoa tamko kuhusu afya ya mwanablogu huyo na pia kuhusu kuahirishwa kwa adhabu yake.
Mashirika ya kutetea haki za binadamu ikiwemo Amnesty Internationalyamesema katika taarifa yao kwamba Badawi alifanyiwa uchunguzi wa kimatibabu na kugundua kwamba uchungu na majereha aliyoyapata kutoka kwa mijeledi ya kwanza bado hazijapona.
Daktari wake alishauri adhabu yake kuahirishwa hadi atakapopata nafuu.
Duka lawabagua wateja wazawa China.Duka moja la nguo mjini Beijing China
limezua mjadala nchini humo baada ya
kuweka maelezo yanayopiwapiga marufuku
wateja wake raia wa Uchina.
Duka hilo limehusishwa katika mgogoro wa
ubaguzi wa rangi baada ya kuweka maelezo
y…Read More
Bi harusi wa miaka 14 ampa sumu
mumeweBi harusi wa miaka 14 nchini Nigeria
ameshtakiwa kwa kuwaua watu wanne
akiwemo mumewe wa miaka 35 baada ya
kuweka sumu ya panya katika chakula
alichoandaa kwa sherehe za haruysi yake.
Kesi hiyo imewashangaza wahaharakati wa h…Read More
0 comments:
Post a Comment