Facebook

Sunday 5 October 2014

Basi la Najimunisa lagongana uso kwa uso na Land Cruiser.

Jana Usiku huu eneo la Darajani  Mbezi
Mwisho,Basi la Kampuni ya Najimunisa
limegongana uso kwa uso la gari ndogo aina
ya Land Cruiser hard Top.

Ajali imetokea majira ya Saa tano usiku,Basi
la Najimunisa likiwa "limetanua" njia likitokea
Mwanza likakutana uso kwa uso na Land
cruiser iliyokuwa katika "sight" yake.
Basi limetumbukia korongoni juu
chini,Majeruhi ni wengi na Polisi
wamelazimika kutumia risasi za moto
kuwatawanya "vibaka" waliotaka kutumia
mwanya huo kuwapora majeruhi wa ajali.
Uokozi unaendelea na majeruhi wengi
wanapelekwa hospital,mpaka sasa hakuna kifo
kilichoripotiwa,Magari ya "BreakDown"
wanajitahidi kulitoa basi chini ya korongo.

Endelea kutembelea www.bantutz.com

0 comments:

Post a Comment