Facebook

Monday 13 October 2014

"Nyuma Ya Pazia" kuzama kwa Meli ya Titanic-Sehemu-Full Article

 Photo: UKWELI KUHUSU TITANIC---- Sehemu ya 1

"Kama ilivyo punje moja ya mchanga mbele ya fukwe za bahari kuu za dunia, ndivyo ulivyo ufahamu wetu mbele ya tusiyoyajua duniani na ulimwenguni na mbele ya yale tunayodhani kuwa tunayajua". 
jambo la kweli kuhusu uhalisi umekuwa ukifichwa mno kwani ukweli una tabia ya kuuma. Na badala yake binadamu wamekuwa wakipenda uongo mtamu uliokolezwa asali kiasi cha kuaminika kama kweli lakini kumbe ni uongo. Hata hivyo tukubaliane kimsingi kuwa kuamini uongo ni kuruhusu fikra zilizo huru kupumbazika na kuvaa ujinga katika imani.
Yapo matukio kadhaa yaliyowahi kutokea hapa duniani na kuwaacha binadamu kwa mshangao, kwa machungu au kwa raha, lakini kutokana na hulka yetu ya kuamini uongo mtamu tumejikuta tukiamini uongo kuhusu matukio hayo badala ya ukweli wenyewe.

Tatizo letu binadamu tulio wengi ni uvivu wa kutokutaka kusaka ukweli na badala yake kwa uvivu tu tunabaki kusadiki uongo ambao unalenga kuficha ukweli. Huo ni upumbavu na kujiruhusu kuwa juha. Kwa leo sitaki kuzungumzia ukweli kuhusu shambulio la WTC, nataka tuzungumzie kuzama kwa meli kubwa kuliko zote zilizowahi kutengenezwa na binadamu duniani, yani Titanic.

Hii ni meli ambayo iliaminiwa na waundaji wake kuwa kamwe haiwezi kuzama kutokana na uimara na usanifu uliotumika kuutengeneza kwa miaka mingi. Ndani ya Titanic kulikuwepo na mahitaji yote muhimu kwa maisha ya nyumbani. Uliweza kucheza soka ndani ya Titanic, uliweza kuogelea, kucheza disko, kununua bidhaa kutoka maduka mbali mbali ndani ya Titanic. Ungeweza kusoma ndani maktaba, baa, mahoteli ya kula na kulala, watu walioa na kuolewa ndani ya meli hii. Kifupi Titanic ilikuwa ni kijiji ndani ya bahari.
Lakini pamoja umaridadi wake, uimara wake, sifa zake, bado Titanic iliweza kuzamishwa ndani ya maji na majasusi!!! 

.........Majasusi Gani, kwa nini.........Fuatilia muendelezo!! kwa kweli nimeamua kuropoka ukweli mchungu!!

"Kama ilivyo 'punje' moja ya mchanga katika fukwe za bahari kuu za dunia, ndivyo ulivyo ufahamu wetu mdogo mbele ya mambo mbalimbali makubwa na mengi tusiyoyajua duniani na mbele ya yale tunayodhani kuwa tunayajua". 

Jambo la kweli kuhusu uhalisi umekuwa ukifichwa mno kwani ukweli una tabia ya kuuma. Na badala yake binadamu wamekuwa wakipenda uongo mtamu uliokolezwa asali kiasi cha kuaminika kama kweli lakini kumbe ni uongo. Hata hivyo tukubaliane kimsingi kuwa kuamini uongo ni kuruhusu fikra zilizo huru kupumbazika na kuvaa ujinga katika imani.

Yapo matukio kadhaa yaliyowahi kutokea hapa duniani na kuwaacha binadamu kwa mshangao, kwa machungu au kwa raha, lakini kutokana na hulka yetu ya kuamini uongo mtamu tumejikuta tukiamini uongo kuhusu matukio hayo badala ya ukweli wenyewe.

Tatizo letu binadamu tulio wengi ni wavivu wa kutokutaka kusaka ukweli na badala yake kwa uvivu tu tunabaki kusadiki uongo ambao unalenga kuficha ukweli. Huo ni upumbavu,ujinga na kujiruhusu kuwa Juha. Kwa leo sitaki kuzungumzia ukweli kuhusu shambulio la "World Trade Center" WTC huku wengi wakilifahamau kama tukio la Septemba 11, nataka tuzungumzie kuzama kwa meli kubwa kuliko zote zilizowahi kutengenezwa na binadamu duniani, yani Titanic.

  Titanic meli ambayo iliaminiwa na waundaji wake kuwa kamwe haiwezi kuzama kutokana na uimara na usanifu uliotumika kuutengeneza kwa miaka mingi. Ndani ya Titanic kulikuwepo na mahitaji yote muhimu kwa maisha ya nyumbani. Uliweza kucheza soka ndani ya Titanic, uliweza kuogelea, kucheza disko, kununua bidhaa kutoka maduka mbali mbali ndani ya Titanic. Ungeweza kusoma ndani maktaba, baa, mahoteli ya kula na kulala, watu walioa na kuolewa ndani ya meli hii. Kifupi Titanic ilikuwa ni kijiji ndani ya bahari.
Lakini pamoja na umaridadi wake, uimara wake, sifa zake, bado Titanic iliweza kuzamishwa ndani ya maji na majasusi!!! 

Photo: UKWELI KUHUSU TITANIC----Sehemu ya 2

Kwa nini waliamua kuzamisha meli hii? Walifanyaje mipango yao kwa siri hadi isigundulike? Endelea kusoma maandiko haya.

Inajulikana kuwa mwanzoni mwa miaka ya 1830 Amerika bado ilikuwa haijawa na Benki Kuu wakati majasusi hawa wa Ki-Italiano maarufu kama Jesuits walihitaji benki nyingine Amerika ambayo wangetumia kuchota  fedha kwa ajili ya kufanikisha mipango yao ya vita na ajenda nyingine za siri duniani kote.

Mnamo mwaka 1910 karibu na pwani ya Georgia katika kisiwa cha Jekyll wanaume saba walikutana kwa lengo la kuanzisha benki hiyo ambayo ingeitwa Benki ya Akiba.
 Hapa ninawazungumzia Nelson Aldrich na Frank Vanderlip ambao waliwakilisha taasisi ya fedha ya tajiri Rockefeller; 
Henry Davison, Charles Norton na Benjamin Strong waliowakilisha kampuni ya J.P, wengine ni Morgan na Paul Warburg waliowakilisha benki ya Uropa ijulikanayo kama Rothschilds.
hawa jamaa walipania kweli kweli na kuna kitu walilenga, wakakaa chini na kuweka mikakati.... ITAENDELEA.Kwa nini waliamua kuzamisha meli hii? Walifanyaje mipango yao kwa siri hadi isigundulike? 

Inajulikana kuwa mwanzoni mwa miaka ya 1830 Amerika bado ilikuwa haijawa na Benki Kuu wakati majasusi hawa wa Ki-Italiano wakishirikiana na wengine kutoka Amerika maarufu kama Jesuits walihitaji benki nyingine Amerika ambayo wangetumia kuchota fedha kwa ajili ya kufanikisha mipango yao ya vita na ajenda nyingine za siri duniani kote.

Mnamo mwaka 1910 karibu na pwani ya Georgia katika kisiwa cha Jekyll wanaume saba walikutana kwa lengo la kuanzisha benki hiyo ambayo ingeitwa Benki ya Akiba.
Hapa ninawazungumzia Nelson Aldrich na Frank Vanderlip ambao waliwakilisha taasisi ya fedha ya tajiri Rockefeller;
Henry Davison, Charles Norton na Benjamin Strong waliowakilisha kampuni ya J.P, wengine ni Morgan na Paul Warburg waliowakilisha benki ya Uropa ijulikanayo kama Rothschilds.
Hawa jamaa walipania kweli kweli na kuna kitu walilenga, wakakaa chini na kuweka mikakati....

Nikuongezee maarifa ewe mpenzi wa "JICHO LANGU LA TATU" Rockerfeller hii ni familia ya kitajiri kubwa sana duniani ambayo inamuabudu shetani,ambayo hadi leo hii inawatu mashuhuri,leo hii sitajikita kuielezea familia hiyo lakini nitakuandalia makala kuhusiana na familia hiyo uweze kujua undani wa familia hiyo ya waabudu shetani.

 Photo: UKWELI KUHUSU KUZAMA KWA TITANIC-----Sehemu ya 3

Ujenzi wa meli ya Titanic ulianza mnamo mwaka 1909 katika karakana ya kutengeneza meli ya Belfast, mji mkuu wa Ireland Kaskazini ukiwa na waumini wengi wa Kiprotestanti ambao walikuwa ni maadui wakubwa wa Jesuits katika harakati Zao humu duniani.

Titanic iliundwa na kumilikiwa na kampuni ya kimataifa ya White Star Line ambayo licha ya Titanic pia ilikuwa na meli kubwa nchini Ujerumani pamoja na Uingereza.

Titanic iliundwa na watu mabilionea na maarufu ambao hawakujihusisha na uundwaji wa Benki ya Akiba na kwa jinsi hiyo J.P Morgan alilazimishwa na Jesuits kufadhili ujenzi wa meli hiyo kama maandalizi ya kaburi kwa ajili ya matajiri na watu hao mashuhuri ambao walikuwa wapinzani wa harakati za Jesuits. (The White Star Line-Ibid, uk.246)

Hii ilitokana na hofu kwa Jesuits kwamba watu hawa wangeweza kutumia umaarufu na utajiri wao kuzuia kuwepo kwa Benki ya Akiba. Na kwa kuwa hawa ni watu ambao walipenda starehe na kuponda raha, ni lazima wangependa kuishi ndani ya Titanic ambayo iliundwa maalumu kama kaburi lao bila kujua.

Matajiri, watu maarufu na wale wote ambao Jesuits walitaka wafe walialikwa kuingia ndani ya meli hii kubwa. Pamoja na watu hao maarufu, watu muhimu zaidi waliolengwa hasa ni matajiri watatu ambao ni Benjamin Guggeenhein, Isador Strauss pamoja na John Jacob Astor aliyeaminiwa kuwa tajiri namba moja duniani.

Hawa ni matajiri ambao fedha zao kwa pamoja kwa wakati huo ulikadiriwa kuwa dola za Kimarekani 500 milioni fedha ambayo kwa thamani ya sasa ni dola za Kimarekani 16 bilioni. 

Majasusi wa jesuits walifanikiwa kuwashawishi matajiri wale watatu hadi kuingia ndani ya paradiso inayoelea.
---ITAENDELEA.

 Ujenzi wa meli ya Titanic ulianza mnamo mwaka 1909 katika karakana ya kutengeneza meli ya Belfast, mji mkuu wa Ireland Kaskazini ukiwa na waumini wengi wa Kiprotestanti ambao walikuwa ni maadui wakubwa wa Jesuits katika harakati Zao humu duniani.

Titanic iliundwa na kumilikiwa na kampuni ya kimataifa ya White Star Line ambayo licha ya Titanic pia ilikuwa na meli kubwa nchini Ujerumani pamoja na Uingereza.

Titanic iliundwa na watu mabilionea na maarufu ambao hawakujihusisha na uundwaji wa Benki ya Akiba na kwa jinsi hiyo J.P Morgan alilazimishwa na Jesuits kufadhili ujenzi wa meli hiyo kama maandalizi ya kaburi kwa ajili ya matajiri na watu hao mashuhuri ambao walikuwa wapinzani wa harakati za Jesuits.Soma kitabu hiki uweze kuijua kiundani kampuni hiyo (The White Star Line-Ibid, uk.246)

Hii ilitokana na hofu kwa Jesuits kwamba watu hawa wangeweza kutumia umaarufu na utajiri wao kuzuia kuwepo kwa Benki ya Akiba. Na kwa kuwa hawa ni watu ambao walipenda starehe na kuponda raha, ni lazima wangependa kuishi ndani ya Titanic ambayo iliundwa maalumu kama kaburi lao bila kujua.

Matajiri, watu maarufu na wale wote ambao Jesuits walitaka wafe walialikwa kuingia ndani ya meli hii kubwa. Pamoja na watu hao maarufu, watu muhimu zaidi waliolengwa hasa ni matajiri watatu ambao ni Benjamin Guggeenhein, Isador Strauss pamoja na John Jacob Astor aliyeaminiwa kuwa tajiri namba moja duniani.

Hawa ni matajiri ambao fedha zao kwa pamoja kwa wakati huo ulikadiriwa kuwa dola za Kimarekani 500 milioni fedha ambayo kwa thamani ya sasa ni dola za Kimarekani 16 bilioni.

Majasusi wa jesuits walifanikiwa kuwashawishi matajiri wale watatu hadi kuingia ndani ya paradiso inayoelea.

SEHEMU YA PILI

Photo: UKWELI KUHUSU TITANIC---- Sehemu ya 1

"Kama ilivyo punje moja ya mchanga mbele ya fukwe za bahari kuu za dunia, ndivyo ulivyo ufahamu wetu mbele ya tusiyoyajua duniani na ulimwenguni na mbele ya yale tunayodhani kuwa tunayajua". 
jambo la kweli kuhusu uhalisi umekuwa ukifichwa mno kwani ukweli una tabia ya kuuma. Na badala yake binadamu wamekuwa wakipenda uongo mtamu uliokolezwa asali kiasi cha kuaminika kama kweli lakini kumbe ni uongo. Hata hivyo tukubaliane kimsingi kuwa kuamini uongo ni kuruhusu fikra zilizo huru kupumbazika na kuvaa ujinga katika imani.
Yapo matukio kadhaa yaliyowahi kutokea hapa duniani na kuwaacha binadamu kwa mshangao, kwa machungu au kwa raha, lakini kutokana na hulka yetu ya kuamini uongo mtamu tumejikuta tukiamini uongo kuhusu matukio hayo badala ya ukweli wenyewe.

Tatizo letu binadamu tulio wengi ni uvivu wa kutokutaka kusaka ukweli na badala yake kwa uvivu tu tunabaki kusadiki uongo ambao unalenga kuficha ukweli. Huo ni upumbavu na kujiruhusu kuwa juha. Kwa leo sitaki kuzungumzia ukweli kuhusu shambulio la WTC, nataka tuzungumzie kuzama kwa meli kubwa kuliko zote zilizowahi kutengenezwa na binadamu duniani, yani Titanic.

Hii ni meli ambayo iliaminiwa na waundaji wake kuwa kamwe haiwezi kuzama kutokana na uimara na usanifu uliotumika kuutengeneza kwa miaka mingi. Ndani ya Titanic kulikuwepo na mahitaji yote muhimu kwa maisha ya nyumbani. Uliweza kucheza soka ndani ya Titanic, uliweza kuogelea, kucheza disko, kununua bidhaa kutoka maduka mbali mbali ndani ya Titanic. Ungeweza kusoma ndani maktaba, baa, mahoteli ya kula na kulala, watu walioa na kuolewa ndani ya meli hii. Kifupi Titanic ilikuwa ni kijiji ndani ya bahari.
Lakini pamoja umaridadi wake, uimara wake, sifa zake, bado Titanic iliweza kuzamishwa ndani ya maji na majasusi!!! 

.........Majasusi Gani, kwa nini.........Fuatilia muendelezo!! kwa kweli nimeamua kuropoka ukweli mchungu!!
Naam matajiri wote walishaingia ndani ya Meli wakiongozwa na John Jacob Astor ambaye kama nilivyosema hapo awali huyu ndiye alikuwa bilionea namba 1 duniani kwa wakati huo,
Hakuna yeyote aliyejua kwamba Meli hii ya kifahari ilikuwa inageuzwa kaburi lao muda mfupi ujao,
Harufu ya damu ilinukia kwa kiila Jesuist aliyekuwa melini,hii inathibitishwa na Edward Smith ambaye alikuwa ni nahodha wa Titanic lakini akiwa ni Jesuit hodari.

Edward Smith amekuwa nahodha kwa miaka 26 akiwa na uzoefu wa kutosha na ruti za bahari ya Atlantiki. Amefanya kazi kwa miaka mingi akiwa ndani ya kampuni ya J.P. Morgan.

Hatimaye ilipofika tarehe 10 Aprili, 1912 Titanic iling'oa nanga chini ya nahodha Edward Smith kwa maelekezo ya mkuu wa shirika la Jesuits Francis Browne ambaye naye alikuwepo ndani ya paradiso hiyo inayoelea.

Mwandishi Eric J. Phelps katika kitabu chake, Vatican Assassin anasema; "Francis Browne aliingia ndani ya Titanic tayari akiwa na kurunzi na kamera ya kupiga picha watakaokufa hasa walengwa".

Si Edward Smith tu, lakini kila Jesuit huamini kwa kiapo kuwa amri ya mkuu wao ni amri kutoka kwa Mungu ambaye ni Bwana wa uhai na mauti. Kwa jinsi hiyo saa na dakika zilipowadia Edward Smith alipokea amri ya kutoka kwa wakuu " KIJANA ZAMISHA HIYO MELI HARAKA" 

Na ndipo Edward akaongeza kasi ya Meli kuelekea usawa ule aliolekezwa na wakuu, na wakati huo ndio Francis Browne alikuwa bize na kurunzi mkononi akiamini Camera yake ingepata picha za maiti nyingi za vibopa muda si mrefu....

 SEHEMU YA 3 (Mwisho)
 UKWELI KUHUSU KUZAMA KWA TITANIC---Sehemu ya 5.(Mwisho)

Kama nilivyosema hapo awali Francis Browne alikuwa bize na kurunzi mkononi akiamini Camera yake ingepata picha za maiti nyingi za vibopa,
 pia nahodha wa meli  Edward Smith alikuwa akikimbiza Meli kuelekea uelekeo tofauti akifuata maagizo ya wakuu(jesuits).
W.C.Brownlee katika kitabu Secret Instructions of the Jesuits, American and Foreign Christian Union uk.143 anaweka wazi kwa kusema; 
"Katika Jesuit, kuua watu wasio na hatia ni ruhusa, hivyo kutekeleza mauaji yoyote ni halali na ni baraka za mbinguni".
Naye R.W.Thomson katika kitabu The Footprints of the Jesuits, Hunt and Eaton uk.54 anaelezea kiapo cha kuwa mwanachama wa Jesuits kwa kusema; 
"Nitajiweka katika kundi la wafu siku zote. Nitakuwa tayari kuondoa uhai wa mtu yeyote hata wa kwangu maadamu tu nimepokea amri kutoka kwa Baba (mkuu wa Jesuits). Nitafanya kazi ya ujasusi kwa uaminifu na makini ya hali ya juu kueneza itikadi zao duniani".

Kasi ya meli ilitisha sana ndipo telegramu za tahadhari zilimiminika kwa nahodha, Pamoja na telegramu zaidi ya nane alizotumiwa Nahodha Edward Smith kubadilisha mwelekeo wa meli, yeye aliendelea kuelekeza Titanic katika barafu iliyoganda chini ya bahari tena kwa kuchochea mwendo mkali kwani alitii amri kutoka wakuu. Ndipo meli "isiyozama" ilipoivaa barafu na kuchanika vipande vipande na kuua wote waliokuwa wamelengwa isipokuwa mke wa  bilionea John Jacob Astor aliyeokolewa na boya.

Haya yanahesabiwa kama mafanikio makubwa ya shirika hilo la kijasusi katika historia yao. Na ilipofika 1913 Benki ya Akiba iliweza kuanzishwa nchini Marekani na miezi minane mbele Jesuits waliweza kutumia fedha kuanzisha Vita Kuu ya kwanza ya dunia na kuua mamilioni ya watu.

Huo ndio ukweli nyuma ya pazia ya kuzama kwa meli maarufu ya Titanic ambayo ni simulizi inayowaliza wengi.
Leonardo Di Caprio amejaribu tu kutupa ladha ya mapenzi katika filamu za dunia ya leo lakini ukweli unabaki wazi TITANIC ilizama na mengi yaliyokuwa nyuma ya pazia.

Labda msomaji anaweza kujiuliza je, hili shirika la Jesuits bado ipo duniani? Mwandishi Bill Hughes anatupa jibu katika kitabu The Secret Terrorists kwa kusema; "Hili ni shirika lililo hai jana, leo na kesho hadi pale utawala wao utakaposimikwa duniani kote".  ...............>>>>MWISHO.

Kama nilivyosema hapo awali Francis Browne alikuwa bize na kurunzi mkononi akiamini Camera yake ingepata picha za maiti nyingi za vibopa,
pia nahodha wa meli Edward Smith alikuwa akikimbiza Meli kuelekea uelekeo tofauti akifuata maagizo ya wakuu(jesuits).
W.C.Brownlee katika kitabu Secret Instructions of the Jesuits, American and Foreign Christian Union uk.143 anaweka wazi kwa kusema;
"Katika Jesuit, kuua watu wasio na hatia ni ruhusa, hivyo kutekeleza mauaji yoyote ni halali na ni baraka za mbinguni".
Naye R.W.Thomson katika kitabu The Footprints of the Jesuits, Hunt and Eaton uk.54 anaelezea kiapo cha kuwa mwanachama wa Jesuits kwa kusema;
"Nitajiweka katika kundi la wafu siku zote. Nitakuwa tayari kuondoa uhai wa mtu yeyote hata wa kwangu maadamu tu nimepokea amri kutoka kwa Baba (mkuu wa Jesuits). Nitafanya kazi ya ujasusi kwa uaminifu na makini ya hali ya juu kueneza itikadi zao duniani".

Kasi ya meli ilitisha sana ndipo telegramu za tahadhari zilimiminika kwa nahodha, Pamoja na telegramu zaidi ya nane alizotumiwa Nahodha Edward Smith kubadilisha mwelekeo wa meli, yeye aliendelea kuelekeza Titanic katika barafu iliyoganda chini ya bahari tena kwa kuchochea mwendo mkali kwani alitii amri kutoka wakuu. Ndipo meli "isiyozama" ilipoivaa barafu na kuchanika vipande vipande na kuua wote waliokuwa wamelengwa isipokuwa mke wa bilionea John Jacob Astor aliyeokolewa na boya.
Haya yanahesabiwa kama mafanikio makubwa ya shirika hilo la kijasusi katika historia yao. Na ilipofika 1913 Benki ya Akiba iliweza kuanzishwa nchini Marekani na miezi minane mbele Jesuits waliweza kutumia fedha kuanzisha Vita Kuu ya kwanza ya dunia na kuua mamilioni ya watu.
Huo ndio ukweli nyuma ya pazia ya kuzama kwa meli maarufu ya Titanic ambayo ni simulizi inayowaliza wengi.
Leonardo Di Caprio amejaribu tu kutupa ladha ya mapenzi katika filamu za dunia ya leo lakini ukweli unabaki wazi TITANIC ilizama na mengi yaliyokuwa nyuma ya pazia.

Labda msomaji anaweza kujiuliza je, hili shirika la Jesuits bado ipo duniani? Mwandishi Bill Hughes anatupa jibu katika kitabu The Secret Terrorists kwa kusema;

 "Hili ni shirika lililo hai jana, leo na kesho hadi pale utawala wao utakaposimikwa duniani kote". 

                                     MWISHO.

Endelea kutembelea www.bantutz.com uweze kusoma makala mbalimbali,"JICHO LANGU LA TATU" nakuletea makala zenye kusisimua kwa kufichua maovu na kukuongezea maarifa mbalimbali ambayo si rahisi kuyapata sehemu nyingine.Bantu Inc iko katika mchakato wa kufungua Social Network ambayo itaanza kufanya kazi mwaka kesho.Nitakuwa na sehemu maalumu kwa ajili ya makala zangu za kuvutia,kusisimua na kufundisha.  

Imeandaliwa na........... 
                                     Katemi Methsela
                                      +255716418657
                                      +255785442107

0 comments:

Post a Comment