Facebook

Monday 13 October 2014

Tanzania yaifumua Benin 4-1

Taifa Stars imeitungua Benin kwa mabao 4-1
katika mechi ya kitarafiki ya kimataifa
iliyochezwa leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini
Dar es Salaam.

Mabao ya Stars yalifungwa na wachezaji wake
wawili wanaokipiga nchini na wawili
wanaocheza nje ya Tanzania.
Nadir Ali Harob ‘Cannavaro’ wa Yanga ndiye
alianza kabla ya Amri Kiemba wa Simba
kuongeza la pili.

Mabao mengine mawili yalifungwa na na
Thomas Ulimwengu kutoka TP Mazembe na
Juma Luizio anayekipiga Zesco ya Zambia.

Stars ilionyesha kiwango kizuri na kuwazidi
ujanja Benin katika mechi hiyo inayotambuliwa
na Shirikisho la Soka la Kimaitaifa.

0 comments:

Post a Comment