Facebook

Wednesday 8 October 2014

WENGER UWEZO UNAO,SABABU UNAYO,IMEBAKI KAZI MOJ TU YA KUMCHAPA ADUI YAKO.


                    Arsenal FC v Galatasaray AS - UEFA Champions League
  Mwaka 1971 nduli amin aliingia madarakani kama Rais wa Uganda,Alimkuta tayari Mwalimu Nyerere ameshakuwa Rais wa Tanzania.Licha ya kuwa Nyerere alimtangulia Iddi Amin kama Rais,Pia Nyerere alikua mkubwa kwa umri kuliko nduli Amin.Lakini hiyo haikuwa sababu ya Nduli Amin kumuheshimu Nyerere.Nduli hakumuheshimu Nyerere kwasababu alikuwa akiionea Tanzania na Nyerere vile atakavyo.Mwaka huo huo wakati anaingia madarakani alijaribu kuvamia Mji magharibi(Kagera),Ingawa hakufanikiwa lakini bado alifanikiwa kuitesa  kidogo Tanzania.
Amin bado akaendelea kumdharau Nyerere na Tanzania yake,Siku moja alimwandikia barua Mwalimu Katika barua hiyo Dada alimmwambia Nyerere hivi  "Nataka nikuhakikishie kwamba nakupenda saana, na  kama ungelikua mwanamke basi ningefikiria jinsi ya kukuoa japo kichwa chako kimejaa mvi. Lakini kwakuwa wewe ni mwanaume basi uwezekano huo haupo". Kwa Kashfa hii Nyerere hakujibu kitu.Bado Amin akaendelea kutembea kifua mbele huku akiamini Tanzania na Nyerere si kitu.Mwaka 1978 Iddi Amin alivamia tena Mji magharibi(Kagera),na kufanikiwa kuuteka Mji,Amin akaendelea kutamba na kusema kuwa alitumia dakika 25 tu kuiteka Kagera.Amin aliendelea 

“ na hii bendera imeandikwa chama cha mupinduzi,lakini mimi nataka nyinyi siku ngine kama maneno itakuwa mbaya nyinyi mtarudi mtasafisha mpaka Dar-es-salaam”.

Baada ya hayo Nyerere uvumilivu ukamshinda
                “Tunayo kazi moja Watanzania, tunayo kazi moja tu, ni kumpiga.Uwezo tunao Sababu tunayo  na Nia tunayo.” 

Hayo ni maneno ya Nyerere baada ya kushindwa kuvumilia maneno na mambo ya Amin anayowafanyia Watanzania.Nyerere akafanikiwa kuiongoza Tanzania kumpiga Amin,Tangu Kupigwa kwake na Nyerere Amin hakusikika tena anaizungumzia Tanzania wala Nyerere.Alimuheshimu Nyerere Baada tu ya Kumpiga.

             Yaliyomkuta Nyerere kwa Amin ni kama kesi  ya Wenger kwa Mourinho.Licha ya Wenger kumzidi Mourinho umri na muda wa kazi lakini Mourinho hamuheshimu wenger hata kidogo.Mourinho anamdharau Wenger kwasababu  kila siku akikutana naye anamfunga,Mpaka sasa ameshamfunga mechi 7 kati ya 12 walizokutana,Tangu Mourinho arejee nchini uingereza kikosi cha  Arsene Wenger akijafunga hata goli moja kwenye lango la Chelsea,Mechi 4 za mwisho Chelsea chini ya Mourinho imeshaifunga Arsena bao 10 huku Arsenal hawajafunga hata goli moja.Unafikiri Mourinho ataanzaje kumuheshimu Wenger?.Kama kila siku akikutana naye anampa kipigo cha uhakika kwanini asitembee kifua mbele dhidi  ya wenger?.Hata mimi ningekuwa Mourinho ningekuwa nina kila sababu ya kumuita Wenger ‘Specialist in Failure’
         Wenger uwezo  wa kufuta aibu anayoipata kutoka  kwa Chelsea na Mourinho anao,Sababu ya kuwa juu ya Chelsea anayo ila anaonekana hana nia tu.Ukiangali Chelsea na Arsenal utagundua ni klabu mbili tofauti.Kwa  Uingereza ukiacha Manchester United hakuna timu nyingine yeyote inayoifikia Arsenal Kiutajiri.Arsenal ina uwezo mkubwa wa kutumia kuliko Chelsea,Lakini leo hii ukiangalia Kikosi cha Chelsea  huwezi kufananisha na cha Arsenal hasilani.Chelsea wana kikosi kilichoshiba.Arsenal kwa utajiri walionao ilibidi wawe na kikosi kizuri zaidi ya Chelsea,Lakini haipo hivyo.Hiyo yote ni kutokana na sera mbovu za usajiri za Arsene Wenger.Sera za Wenger ndio zinamponza kila siku kupigwa na kunyanyasika na timu zinazofanya usajiri mzuri kuliko yeye.
                  Mourinho ana Costa Wenger ana Welbeck,Kati ana Matic wakati wenger ana Flamin,Hiyo ndio  tofauti yao huo ndio ujinga unaomfanya Wenger aendelee kuwa ‘kubwa jinga’kwa Mourinho.Wenger hana ujanja zaidi ya kutumia pesa nyingi kuwaleta wakina khedira na Cavani kama kweli ana nia ya kuondokana na aibu anayopata kila siku kutoka kwa Mou.
              Wengi watapinga na kuniambia wenger hana sababu ya kufanya usajili kwa ajili ya kumfunga Mou tu,Hapo Mou nimemtolea mfano tu.Maana yangu kubwa Ni kuwa Wenger  lazima afanye usajiri wa Nguvu ili aweze kushindana na timu nyingine kubwa zenye kaliba ya Arsenal  kama Bayern,United,Madrid na Barcelona.Timu hizo nne ukijumlisha na Arsenal ndio timu 5 Tajiri Duniani lakini timu nne ni tofauti kabisa na Arsenal ndani ya uwanja.
            Wenger inabidi awe na nia ya dhati kama Nyerere  ya kuondoka kwenye utumwa wa kuonewa na nduli iddi Amin. Wenger Uwezo anao,Sababu anayo ila hana budi kubadilishe nia yake  kwa kuanza kutumia utajiri wa arsenal ipasavyo ili aende sawa na wapinzani wake.Wenger kama anataka heshima yake irudi ni lazima aanze tena kuwaadabisha wapinzani wake.Ferguson alikua akimuheshimu Wenger kwasababu alikua akimchapa.Ndani ya miaka 10 ya kwanza ya Arsene wenger  ndani ya Arsenal alikua amemfunga mechi nyingi Fergi kuliko Fergi alivyomfunga yeye.Hiyo ilikua sababu tosha ya Fergi kumuheshimu.Lakini mou hatamuheshimu wenger mpaka pale atakapomchapa.

Endelea kutembelea www.bantutz.com uweze kusoma makala mbalimbali zilizoandikwa na waandishi makini wanaofuata weleni katika uandishi.Bantu Inc iko katika mchakato wa kufungua Social Network kubwa na ya kisasa "Kaa Mkao wa Kula".
Imeandaliwa na.....................
             Allen kaijage
             0655106767
                     Kaijagejr@gmail.com

0 comments:

Post a Comment