Facebook

Tuesday 7 October 2014

Steve Jobs is Apple Inc,Apple inc is Steve Jobs "iGenius"

Top 5 CEO of tech companies

Binadamu tunaamini maisha ya mwanadamu hubadilika kutokana na mazingira,lakini mazingira hayo yanamtegemea mwanadamu kwa namna moja au nyingi,inamaana hivi ni vitu viwili vinavyotegemeana,Mwanadamu anayategemea mazingira na mazingira yanamtegemea mwanadamu.
Katika Ulimwengu wa leo kitu kikubwa kinachobadilisha maisha ya binadamu ni teknolojia,teknolojia ndiyo inayobadilisha mazingira ya mwanadamu hivi sasa,Mfano mzuri Misri waliweza kuitumia teknolojia na kuligeuza jangwa kuwa ardhi nzuri kwa ajili ya kilimo kupitia "Irrigation Technology".Vivyo hivyo Iran waliweza kutumia teknolojia ya Nyuklia kuligeuza jangwa kuwa ardhi nzuri kwa ajili ya makazi ya binadamu na shughuli nyinge muhimu.

Binafsi huwa napenda sana kufuatilia masuala ya teknolojia,Kuna kampuni nyingi sana za teknolojia duniani lakini kuna baadhi ya kampuni zilianzishwa zikadumu kwa kipindi kifupi kisha zikaanguka,lakini pia kuna kampuni zilizosimama kidete tangia zilipoanzishwa hadi leo hii zinafanya mambo makubwa na ya ajabu pasipo kutegemea.Kikubwa unapoona kampuni hizo zinasimama na kuwa imara zaidi katika utengenezaji wa bidhaa zake na soko kwa ujumla huwa kuna jopo la watu nyuma yake,na jopo hilo pia linakiongozi wake,hao viongozi ni huitwa wakarugenzi  kwa lugha ya kimombo wanaitwa "Chief Executive Officers-C.E.O" 

Hawa ndio watu muhimu sana katika kampuni yoyote ile.Kuna baadhi ya ma-C.E.O ambao wameweza kuziongoza kampuni katika mstari ulionyoka wa mafanikio,wa kwanza anaitwa Jeffrey P. Bezos ambaye ndiye anaiongoza kampuni ya Amazon.com iliyoenea dunia nzima na kuajiri watu zaidi ya Milioni 30 huku wakiibadili dunia kwa kurahisisha biashara zinazofanyika kwa njia ya mtandao E-Commerce,Yun Jong-Yong anayeongoza kampuni ya Samsung Electronics yenye makao makuu yake nchini Korea Kusini ama kwa hakika mageuzi yaliyofanywa na Samsung Group dunia nzima yanatambulika hivi sasa katika soko la teknolojia wanatengeneza vifaa vya kila aina Simu,Tv,Computer n.k.Watatu ni mwanamama Margaret C. Whitman anayeongoza kampuni ya kutengeneza Computer duniani Hawlett-Packard {HP},John T Chember anayeongoza kampuni ya IBM-International Business Machines  inayojishughulisha na utengenezaji wa vifaa mbalimbali vya kielectroniki zikiwemo Super Computer,Business Mchines,kadi za benki,Computer maalum kwa ajili ya matumizi ya Kampuni au kikundi fulani.Lakini katika orodha hii siwezi kumuacha mtu muhimu sana ambaye ameleta mageuzi makubwa sana katika nyanja ya mawasiliano hususan katika simu za mkonon na Sekta nzima ya muziki duniani,huyu si mwingine bali ni Steve Jobs watu wengi Nchini Marekani wanamuita "iGenius" au iC.E.O

Leo hii katika "JICHO LANGU LA TATU"  linaiangazia nyota iliyoibuka February 24, 1955 San Francisco, California huko Marekani mjasiriamali,mwanzilishi,mkurugenzi,mwenyekiti na mvumbuzi wa kampuni ya Apple Inc huyu anaitwa Steven Paul "Steve" Jobs .
 Steve Jobs alikuwa ni Mmarekani mwenye asili ya Syria kwani baba yeke mzazi Abdulfattah "John" Jandali ni Msyria aliishi Marekani kwa muda mrefu na Mama yake Joanne Carole Schieble ni Mswisi aliyeishi pia Marekani kwa muda mrefu na wawili hao walikutana walipokuwa wanasoma huko California Marekani lakini wawili hao walikataliwa kuoana na wazazi wao.Lakini walipofariki wazazi wa Steve Jobs waliweza kuona na kuzaa mtoto mwingine aitwaye Mona.Lakini baada ya miaka mitano ndoa ya wazazi wa Steve Jobs ilivunjika.

Steve Jobs alilelewa na mama yake ambaye alikuwa hana uwezo wa kumsomesha Steve,hapo baadae aliamua kwenda kumkabidhi Steve Jobs kwa familia ya kitajiri ya Bwana Paul Reinhold Jobs (1922–1993) na mkwa wake Clara Jobs (née Hagopian) (1924–1986) ambao waliishi kwa muda mrefu bila kupata mtoto hivyo basi walimfanya Steve Jobs kuwa mtoto wao wa kipeke ambae walimpaa kila anachokihitaji.Familia ya Jobs ilihama kutoka San Francisco na kwenda kuishi Mountain View, California wakati Steve Jobs akiwa na miaka 5.Familia ya bwana Jobs ilifanikiwa kumiliki Gereji na Duka kubwa la utengenezaji wa radio mbovu seheme ambazo Steve Jobs alitumia muda wake mwingi kujifunza vitu mbalimbali hususan masuala ya elektroniki.Huku baba yake wa Kuasili alitumia muda mwingi kumfundisha Steve Jobs jinsi ya kuvirekebisha na kutengeneza vifaa vya kielektroniki kama Redio na runinga,kuanzia kipindi hicho Steve Jobs akawa na mapenzi makubwa katika vifaa vya kielektroniki.Mama yake,Clara alikuwa ni mhasibu alikuwa anamfundisha Steve Jobs kila siku hesabu kabla hajaenda Kazini.
 Home of Paul and Clara Jobs, on Crist Drive in Los Altos, California.
Baada ya kumaliza elimu ya awali Monta Loma Elementary school huko Mountain View,alipelekwa katika shule ya Cupertino Junior High na Homestead High School huko Cupertino,California.
Historia kubwa ya Steve Jobs katika masuala ya teknolojia ikaanzia hapa kwani alikutana na Bill Fernandez,jirani yake na rafiki yake pia ambaye wote kwa pamoja walikuwa wanapenda masuala ya elektroniki,Fernandez akamtambulisha Steve Jobs kwa rafiki yake mkubwa Steve Wozniak,kijana aliyebobea kwenye masuala yaa Computer na elektroniki "A Computer and technological Whiz Kid" alimaarufu kama "Woz"

Mwaka 1969 Wozniak na Fernandez walitengeneza Computer ambayo ilikuwa haijakamilika na kuiita "The Cream Soda Computer" ambayo walimuonyesha Steve Jobs na alivutiwa nayo sana.Wozniak na Fernandez waliita Computer hiyo Cream Soda Computer kwa sababu walikuwa wanapenda sana kunywa Cream Soda kipindi wanaitengeneza.
Lakini mwaka 1972 walifanikiwa kumaliza chuo na Steve Jobs alifaulu na kwenda kusoma Reed College huko Portland, Oregon,chuo ambacho kilikuwa na gharama sana lakini wazazi wake wakitafuta pesa kwa hali na mali ili waweze kumsomesha,wahenga wanasema ng'ombe wa masikini hazai,kauli hii ilitimia kwani baada ya miezi 6 tu Steve Jobs alifukuzwa chuo na alitumia takribani miezi 18 akijishughulisha na kazi za uvumbuzi na uchunguzi wa vitu mbalimbali katika masuala ya elektroniki.

Mwaka 1974 Steve Jobs alisafiri na kwenda India sehemu ambayo alikuwa anakwenda kwa wataalamu mbalimbali wa masuala ya elektroniki kwa watu kama Neem Karoli Baba, Daniel Kottke na baada ya kuishi India kwa muda wa miezi 9 alirudi Marekani,na akaenda kujiunga katika kampuni ya Atari iliyokuwa  chini ya Mmarekani aliyekuwa tajiri sana kwa kipindi hicho aitwaye Bushnell, na kumpa kazi ya kutengeneza circuit board kwa ajili ya kutengeneza  "arcade video game Breakout"
 Kampuni hiyo ilikuwa inamlipa $100 kwa kila "Chip" moja iliyokuwa inaingizwa kwenye mashine
 Steve Jobs alikuwa ni mtaalamu sana kwenye utengenezaji wa "Circuit board and design" kitu kilichomvutia tena rafiki ya muda mrefu Wozniak ambaye alimuangalia Jobs kwa jicho la husuda akiwa katika kampuni ya Atari,kisha akamfuata na kuingia nae  makubaliano ya kutengeneza "Chip" ambazo ni ndogo zaidi ya zile za kampuni ya Atari.

Hapo ndipo urafiki wao ukarudi tena baada ya kuwa mbali kwa muda mrefu,Steve Jobs alikuwa mzuri sana na hodari katika masuala ya utengenezaji wa fedha kwani alifundishwa vyema na Mama yake Clara namna ya kuwa mjasiriamali.Kupitia zile "Chip" zilizotengenezwa na Steve Jobs, marafiki hao wawili walitengeneza kifaa kilichowezesha mawasiliano ya simu kwa watu waliombali bila gharama yoyote "free long-distance calls" kupitia kifaa kilichoitwa "blue box".Kupitia teknolojia hiyo Steve Jobs na Wozniak walijipatia umaarufu mkubwa ingawa huduma ya bure ilikuwa inapigwa sana vita nchini Marekani,baadae Steve Jobs aliamua kuuza teknolijia hiyo hapo ndipo wazo la kufanya biashara na kujipatia kipato kupitia teknolojia likaanza kuja. Marafiki hao wawili wakaamini kupitia elektroniki wanaweza kushindana na makampuni makubwa na kuyashinda.
Kuanzia mwaka 1975 Steve Jobs na Wozniak wakaanza kuhudhuria mikutano mbalimbali ya masuala Homebrew Computer Club.Steve Jobs alikuwa anapenda sana kazi anazozifanya Edwin H. Land ambaye ndiye mgunduzi wa "Instant Photography" na mwanzilishi wa kampuni ya Polaroid Corporation.

Mwaka 1976 Steve Jobs na rafiki yake Wozniak walifungua kampuni ya biashara na kuiita "Apple Computer Company" ikiwa kama ni kumbukumbu ya majira joto kipindi ambacho wanapenda kuchuma na kula matunda aina ya "Apple" pamoja na mwaka 1976 walitengeneza Computer ya kwana na kuiita  Apple I computer huku pia mwaka huo huo wakapata ufadhili kutoka kwa mfanyabiashara mkubwa aitwaye  Mike Markkula.Ili waweze kupanua wigo wa biashara yao wakaanza kuongeza watu wenye utaalamu mbalimbali mfano mzuri ni mwaka 1978 walipomchukua  Mike Scott kutoka National Semiconductor,John Sculley kutoka Pepsi-Cola.
 

  Logo ya kwanza ya kampuni ya Apple ya baada ya kutengeneza Apple I Computer

Steve Jobs alimuuliza John Sculley swali hili kipindi anajaribu kumshawishi kuhamia katika kampuni ya Apple 

 "Do you want to spend the rest of your life selling sugared water, or do you want a chance to change the world?"

Mwaka 1980 Steve Jobs alianza kuona matunda ya kampuni hiyo baada ya kufanikiwa kutengeneza  Xerox PARC's mouse-driven graphical user interface,ambayo ilisaidia katika utengenezaji wa Computer aina ya  Apple Lisa na mwaka mmoja baadae Apple walitengeneza Computer zilizoleta mageuzi dunia nzima aina ya Macintosh.Apple ikawa kampuni kubwa huku ikawa na watu wengi.Steve Jobs alionekana mtu jeuri na mkali sana kwa wafanyakazi wa kampuni hiyo kitu kilichopelekea hapo baadae kuombwa ajiuzulu na iliyokuwa kamati kuu ya kampuni hiyo ikiongozwa na Sculley ambao walionekana kugombea madaraka ya kampuni hiyo. May 24, 1985 Steve Jobs alijiuzulu rasmi na kujitoa katika kampuni ya Apple.
gallery-thumb
 Steve Jobs akizitambulisha Macintosh Computer kwa mara ya kwanza.


Baada ya kujiondea Apple Steve Jobs alijaribu kujiingiza kwenye masuala ya anga lakini alishindwa na hapo baadae kutokana na uwezo mkubwa aliokuwa nao katika masuala ya teknolojia,alipata machungu sana na kuamua kufungua kampuni yake binafsi aliyoiita  NeXT Inc. mwaka 1985 akiwa na mtaji wa $7milion na mwaka uliofata aliishiwa fedha lakini alifanikiwa kumvutia muwekezaji aliyekuwa ni bilionea kwa kipindi hicho aliyeitwa Ross Perot ambaye aliwekeza vilivyo katika kampuni hiyo.Mwaka 1990 Steve Jobs alifanikiwa kurudi kwenye soko la elektroniki kwa nguvu kubwa sana baada ya kutengeneza Computer alizoziita Next WorkStation alizoziuza kwenye makampuni makubwa,katika shule,vyuo,kwa wanasayansi,kutokana na kuwa na tabia mbalimbali huku Computer moja ikiuzwa $9,999.
Mwaka uliofuata Steve Jobs aliweza kutengeneza Computer iliyokuwa na uwezo wa kukubali teknolojia iliyogunduliwa na Mtaalamu The Berners Lee aliyegundua WWW-World Wide Web,teknolojia iliyoleta mageuzi makubwa duniani hadi hivi sasa hasa katika matumizi ya Internet.


             NexT Workstation ikiwa na Keyboard,Mouse na Next Megapixel Monitor


 Steve Jobs hakuishia hapo kwani mwaka huo huo alitoa toleo jipya la Computer hizo huku zikiwa na uwezo wa kuwasiliana kati ya Computer moja na nyingine kwa njia ya sauti,picha,michoro na video kwa kutumia email kwa mara ya kwanza huku teknolojia hiyo ya email akiita Nextmail Multimedia email System na Computer hizo akiziita Second Generation NextCube na mwaka 1993 baada ya kuuza zaidi ya Computer 50,000 kampuni hiyo iliendelea na kuanza kutengeneza Software zilizoitwa NeXTSTEP/Intel.Kampuni hiyo kwa mara ya kwanza walitanganza faida ya $1.03 million mwaka 1994.Huku mwaka 19954 NeXT Software Inc,  walitengeneza software nyingine iliyoitwa WebObjects ambayo dhumuni lake ni "framework for Web application development".Hakika alikuwa ni mtu wa kipekee sana,kupitia teknolojia hiyo Steve Jobs alijizolea umaarufu mkubwa hadi ikafikia hatua wapinzani wake wakubwa Apple "walimnyooshea mikono" kwa namna alivyoweza kuwagaragaza katika soko la  teknolojia.

Kuna msemo huwa naupenda sana kuutumia mara kwa mara niliukuta katika vitabu mbalimbali vya kihistoria vinavyoelezea Historia ya Ulaya na Afrika,unasema kuwa "If you Can't Beat them,Join Them" Hicho ndicho kitu walichokifanya Apple Inc baada ya kunyanyaswa vibaya na kukosa ubunifu na maarifa katika kutengeneza vifaa mbalimbali vya elektroniki.Kwani mwaka 1997 Apple waliomba kushirikiana na Steve Jobs na wakaomba kutumia Software mbalimbali za Steve Jobs.WebObjects software kwa mara ya kwanza Chini ya Mtaalamu Steve Jobs aliweza kuiingiza software hiyo na kuifanyisha kazi katika Apple Store,MobileMe services,na iTunes Store.

Baada ya kufanya mageuzi makubwa Steve Jobs aliinunua kampuni iliyoitwa Graphics Group ambayo aliibadili jina na kuiita Pixar kutoka kwa kampuni ya Lucasfilm's computer graphics division,alitumia kiasi cha $10 million,huku akitumia $5milion kama mtaji wa kampuni hiyo.Baada ya kuinunua kampuni hiyo matajiri wa kampuni ya Disney wakiongozwa na Michael Eisner waliona umuhimu wa kushirikiana na kampuni ya Pixar iliyokuwa inaandaa sinema mbalimbali na wao walijihusisha katika utengenezaji wa vipindi mbalimbali zikiwemo "Cartoon",Disney ilijizolea umaarufu mkubwa duniani baada ya kushirikiana na Steve Jobs kwani aliweza kuwatengenezea Software mbalimbali kutokana na ubunifu mkubwa na wa hali ya juu aliokuwa nao,hatimaye baada ya kupata faida kubwa sana Disney walifungua kituo chao kikubwa cha kuandalia na kurushia matangazo na vipindi mbalimbali katika sehemu waliyoiita DisneyLand na wakafungua Disney Channel inayofanya kazi hadi hivi sasa.
Mwaka 2003 na 2004 mkataba kati ya Disney na Pixer ulimalizika huku Steve Jobs akikataa kuongeza mkataba mwingine na kampuni huyo iliyokuwa chini ya Michael Eisner.Disney nayo iliisaidia Pixar katika kusambaza sinema mbalimbali zilizokuwa zinatengenezwa na kampuni hiyo,lakini mwanzoni mwa mwaka 2004 Pixar ilisema itatangaza kampuni ambayo watashirikiana katika usambazaji wa sinema zao.
Lakini mnamo  Octoba 2005,baada ya Bob Iger kuchukua nafasi ya Eisner kama mkurugenzi mtendaji wa Disney,kampuni ya Steve Jobs Pixer ilitangaza kushirikiana kwa mara nyingine tena na kampuni ya Disney.Huku Januari 24, 2006, Bob Iger na Steve Jobs walitangaza kampuni ya Pixer   kununuliwa na kampuni ya Disney kwa gharama ya $7.4 billion kitu kilichopelekea Steve Jobs kuwa mshika dau (shareholder) mkubwa katika kampuni ya The Walt Disney Company's kwa 7% huku Bob Iger akiwa na 1.7% na mwanafamilia wa kampuni ya Disney aliyekuwa mshika dau kwa 1% hali iliyompelekea kumlaumu Iger kushirikiana na Steve Jobs.

Tukirudi katika kampuni ya Apple ambayo iliomba kushirikiana na Steve Jobs hapo baadae tena waliomba kuinunua kampuni ya Steve Jobs NeXT kwa $427 million na mwaka 1998 kampuni ya Apple iliweza kumshawishi Steve Jobs aweze kurejea katika kampuni hiyo iliyopoteza nguvu ya ushindani katika soko na hatimaye Steve Jobs alirejea na kuwa Mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo huku wakimtimua Gil Amelio,
Steve Jobs alipopewa tu madaraka ya kuiongoza Apple kwa mara ya pili aliziunganisha kampuni mbili, yake na Apple na kuwa kitu kimoja huku akipiga kapuni baadhi ya "Project" mbalimbali zilizokuwa zinafanyiwa kazi na Apple kama vile Newton, Cyberdog, na OpenDoc
Kwa mara ya kwanza Steve Jobs aliweza kutumia Software alizokuwa nazo kama  NeXTSTEP akatengeneza Mac OS X, na akatoa Computer zilizoitwa iMac ,mageuzi hayo na yaliongeza mauzo ya vifaa mbalimbali vya kampuni hiyo.Dunia nzima ilianza kununua vifaa kutoka kampuni ya Apple makampuni makubwa walipelekea oda kutengenezewa vitu mbalimbali,mwaka 2000 alitoa software iliyoitwa Macworld Expo, Steve Jobs alijizolea umaarufu mkubwa na akakabidhiwa moja kwa moja jukumu la kuiongoza kampuni hiyo na kuanzia hapo akapachikwa jina  "iCEO".
Full-length portrait of man about fifty wearing jeans and a black turtleneck shirt, standing in front of a dark curtain with a white Apple logo
Baada ya mageuzi hayo Steve Jobs alikuwa na akili ya kuona mbali,alikuwa mbunifu na kiongozi mwenyemaono hali ya juu kwani ukiachana na utengenezaji wa Computer pekee alidhamiria kutengeneza vifaa mbalimbali vya kidigitali kama simu na vifaa vya kusikilizia muziki.Alifanikiwa kuingoza Apple kutengeneza iPod portable music player, iTunes digital music software, na the iTunes Store,Vilileta mageuzi makubwa duniani hususan nchini Marekani kwani aliweza kuviunganisha vitu viwili kwa wakati mmoja,mageuzi ya vifaa vya kusikilizia muziki na elektroniki.Steve Jobs alisimama kidete kataika suala la Mageuzi kwenye tasnia ya muziki duiniani hususan kwa wasikilizaji,aliweza kuiongoza Apple kutengeneza iPod mbalimbali iPod classic, iPod Touch, video-capable iPod Nano, screenless iPod Shuffle.

Hakika penye nia pana njia mwaka June 29, 2007 kampuni ya Apple iliingia rasmi katika biashara ya Utengenezaji wa simu za mkononi huku akiunganisha kwa pamoja teknolojia hiyo na ile ya iPod na hatimaye Apple walitengeneza simu aina ya  iPhone,ikiwa na Browser yake inayojitegemea,mageuzi hayo yaliishangaza dunia,Apple ilijozolea umaarufu mkubwa kupitia bidhaa zake za Iphone,mwaka mmoja baadae wakatoa iPhone 3G,ikiwa na mabadiliko makubwa matatu GPS, 3G data and tri-band UMTS/HSDPA. June 2009, wakatoa iPhone 3GS, ikiwa na mabadiliko katika utumiaji wa sauti mbalimbali,kamera ikaongewa uwezo,processor yenye kasi ya hali ya juu.2010 wakatoa iPhone 4 ambayo waliiboresha kwa kuwa nyembamba,kamera yenye 5megapixel ikiwa na uwezo wa kurekodi 720p HD na ikawa na kamera ya mbele kwa ajili ya "Video Calls".October 2011 kampuni ya Apple wakatoa  iPhone 4S.Hayo ndiyo yalikuwa mapinduzi ya Steve Jobs aliyeweza kuibadili Computer na kuwa simu ya mkononi.


Shoulder-high portrait of two middle aged men, the one on left wearing a blue dress shirt and suitcoat, the one on right wearing a black turtleneck shirt and with his glasses pushed back onto his head and holding a phone facing them with an Apple logo visible on its back
Steve Jobs akimuonyesha iPhone 4 Rais wa Urusi Dmitry Medvedev  June 23, 2010

Licha ya mageuzi na ubunifu mkubwa sana aliokuwa nao Steve Jobs lakini kuna kitu kilichokuwa kinamsumbua kwa muda mrefu,kitu kilichokuwa kinamnyima raha na amani,ilikuwa ni ugonjwa wa kansa au saratani aliokuwa nao katika mfumo wa Chakula hususan Tumboni,kwani mwaka 2003 Steve Jobs aligundulika ana ugonjwa wa kansa na aliweza kupata tiba mbalimbali katika vipindi tofauti tofauti,huku alitumia zaidi vitu vya asili kama matunda na Juisi,vilevile mionzi ili kupunguza madhara ya ugonjwa huo.Huku mwaka 2009 alijipunguzia majukumu katika kampuni ya Apple huku shughuli nyingi alikuwa akimuongoza Tim Cook aliyekuwa msaidizi wake aweze kuzifanya.Ilipofika mwaka 2011 mwanzoni afya yake ilianza kuzorota,Lakini aliweza kuhudhuria katika uzinduzi wa  iPad 2, Machi,2,2011.




Sehemu aliyokuwa anaishi Steve Jobs na familia yake Palo Alto-Marekani

Steve Jobs alitangaza rasmi kujiuzulu kama C.E.O wa Apple Inc August 24, 2011.Steve Jobs aliandika hiki.........
"I have always said if there ever came a day when I could no longer meet my duties and expectations as Apple’s CEO, I would be the first to let you know. Unfortunately, that day has come."

Jobs alijivua majukumu yote na kumkabidhi Tim Cook na yeye akibaki kama mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya Apple Inc hadi baada ya wiki sita zilizofuata ambapo alifariki dunia.
Ilikuwa ni kama nyota iliyowaka na kuzimika ghafla akiacha majonzo na simanzi kubwa katika Ulimwengu wa teknolojia.Ilikuwa saa 9 usiku akiwa katika makazi yake huko Palo Alto, California,Steve Jobs alifariki dunia baada ya safari ya muda mrefu yenye milima na mabonde lakini aliweza kukitumia vyema kipawa chake katika kuleta mabadiliko duniani.


Baada ya kifo chake kampuni kubwa duniani za Apple Inc,Microsoft na Disney zilipeperusha bendera zake nusu mlingoti katika makao makuu ya kampuni hizo kama heshima na kuomboleza kwa pamoja baada ya kifo cha shujaa Steve Jobs.


Wananchi mbalimbali nchini Marekani walipeleka maua pamoja na bidhaa mbalimbali za kampuni ya Apple kama vile iPad na iPhone nje ya duka kubwa la kampuni hiyo kama ishara ya maombolezo na heshima kwa muasisi wa kampuni hiyo.

Vyombo vyote vya habari ulimwenguni vilishinda vinaonyesha moja kwa moja matukio mbalimbali ya msiba huo,magazeti,vituo vya Runinga,radio na mitandao ya kijamii habari kubwa ilikuwa ni kifo cha "iGenius" Steve Jobs.

Viongozi mbalimbali ulimwenguni walituma salamu zao za rambirambi kwa kampuni ya Apple Inc,Disney na kwa familia ya Steve Jobs.Huku Rais wa Marekani,Barrack Hussein Obama,Waziri mkuu wa Uingereza,David Cameroon,mwanzilishi wa Microsoft Bill Gates na wengine wengi walituma salamu zao za rambirambi.

Lakini rafiki wa Steve Jobs,Bw.Steve Wozniak waliyesoma pamoja na baadae kufungua kampuni pamoja alihuzunishwa sana na kifo cha rafiki yake mkubwa alimbatiza jina na kumuita iGenius.

Simanzi ilitawala dunia nzima hususan katika kampuni ya Apple ambao waliomboleza kifo cha Steve Jobs kwa kusitisha shughuli zao mbalimbali.

Hakika dunia iliweza kunifaika kupitia kwa "iGenius" huyu alifanya mambo ya kuustajabisha dunia dunia pale alipounganisha kwa pamoja teknolojia ya "Projector" na Simu za iPhone kutengeneza simu ambayo ni "Transparent" lakini kwa bahati mbaya alifariki kabla hajakamilisha simu yenye teknolojia hiyo,lakini waswahili husema safari moja huanzisha nyingine Apple Inc hivi sasa iko chini ya Mtaalamu na "Genius" mwingine aliyeshirikiana vyema na Steve Jobs baada ya kurejea katika kampuni hiyo,huyu si mwingine bali ni Tim Cook ambaye aliahidi kuendeleza pale alipoishia Steve Jobs,hakika Apple iko katika mikono ya mtu salama,na hivi sasa kampuni hiyo wametoa toleo jipya la simu zinazoitwa iPhone 6.Tukiwa tuanasubiria ahadi ya Tim Cook kumalizia utengenezaji wa iPhone ambaye ni transpalent yenye uwezo wa Projector.

"Maisha yanakwenda kasi siku zinazidi kusogea lakini mashujaa hawatasaulika kamwe duniani hapo juu ni sanamu ya "iGenius" iliyowekwa katika makao makuu ya kampuni ya Apple Inc.


Imeandaliwa na.......
                                 Katemi Methsela
                               +255716418657
                               +255785442107

Endelea kutembelea www.bantutz.com,Lakini hivi karibuni tutawaletea Social network kubwa na ya kisasa yenye kila kitu na patakuwa na sehemu maalumu kwa ajili ya makala zangu za "JICHO LANGU LA TATU".

0 comments:

Post a Comment