Facebook

Saturday 25 October 2014

VAN GAAL :MOURINHO AMEJIJENGA MWENYEWE


Meneja wa Manchester United Louis van Gaal
amesisitiza kuwa hajafanya lolote kubwa
kusababisha Jose Mourinho kuwa moja ya
makocha wenye mafanikio duniani.
Mourinho, ambaye ni meneja wa Chelsea kwa
sasa, alifanya kazi chini ya Van Gaal akiwa
Barcelona, na huwa anasema Van Gaal na Bobby
Robson ndio wamempa mafanikio.
"Huwa ananitaja mimi na Bobby Robson, na
ninakubali hilo, lakini mambo haya unayafanya
mwenyewe," amesema Van Gaal.
Wawili hao walikutana kwa mara ya kwanza
miaka 17 iliyopita wakati van Gaal alipompa kazi
Mourinho, wakati huo akiwa na miaka 34, kama
mmoja wa makocha wake Nou Camp.
Manchester United inayoongozwa na Louis van
Gaal, inapambana na Chelsea siku ya Jumapili.

0 comments:

Post a Comment