Facebook

Friday 24 October 2014

Taarifa kamili kuhusu Chid Benz kukamatwa na madawa ya kulevya uwanja wa Ndege

Kuna taarifa zilitoka BantuTz.com leo
jioni kuhusu msanii wa muziki wa kizazi kipya
Chidi Benz kukamatwa na dawa za kulevya
katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa
Julius Nyerere Dar es Salaam akiwa anaelekea
Mbeya kwenye show ya Instagram Party
ambayo inatarajiwa kufanyika kesho.
BantuTz.com iliahidi kuzifatilia hizi taarifa
kwa Polisi ili kupata uthibitisho ambapo
imefahamika ni kweli msanii huyu
amekamatwa leo mchana akiwa katika
sehemu ya kuondokea uwanjani hapo
ambapo baada ya alifanyiwa upekuzi na
kubainika amebeba dawa hizo ambapo ni
kete 14 za dawa za kulevya kwenye mfuko wa
shati lake na misokoto miwili ya bangi.
Kwenye mahojiano
kamishna msaidizi wa Polisi (ACP) Hamisi
Selemani ambae ni kamanda wa polisi katika
viwanja vya ndege Tanzania amethibitisha
kukamatwa kwa Chidi Benz na kusema msanii
huyu alipohojiwa amekiri kweli kuwa dawa
hizo ni zake.
Amesema ‘Alikuja Airport kwa ajili ya safari
kwenda Mbeya, kete hizo 14 za dawa za
kulevya zilikua zimefungwafungwa na nailoni
na pia amekutwa na vifaa vingine
vinavyohusiana na watu wanaotumia dawa za
kulevya, kuna kigae na kijiko na yeye
mwenyewe anakiri ni vitu vyake huwa
anatumia ila anashangaa ni kwa nini
vimeweza kubaki kwenye mfuko, tutamfikisha
Mahakamani baada ya kuweza kubaini ni
dawa aina gani za kulevya’

Endelea kutembelea www.bantutz.com kufahamu kila kitakachokuwa kinajiri.

0 comments:

Post a Comment