Facebook

Friday 10 October 2014

Basher Othman-Kiongozi mwenye Umri Mdogo zaidi Duniani.

 
Akiwa na umri wa miaka 16 tu, amefanikiwa kuingia katika serikali ya Palestina akiwa kama Waziri wa Utawala wa Ndani. Binti huyu aliezaliwa mwaka 1998 aliweza kuliongoza jimbo lake la Allar kama Meya kwa kipindi cha miezi 3 kabla hajateuliwa kuwa Waziri.

Je huyu ni nani?
Anaitwa Bashaer Othman, binti wa Kipalestina aliezaliwa tarehe 17 Agosti 1998 katika jimbo la Allar lililopo katikati ya mkoa wa West Bank Hills nchini Palestina. Anaweza kuwekwa katika kundi la watu wenye upembuzi na upeo mkubwa wa vitu (Gifted People) kutokana na uwezo wake mkubwa alionao katika uvumbuzi na upambanuzi wa vitu tofauti tofauti  kwenye jamii yake katika umri mdogo alionao. Uwezo wake katika maamuzi na kipaji cha uongozi alivyonavyo binti huyu ndio vilivyomfanya aishie Elimu ya Sekondari kabla ya kuchaguliwa na wananchi wake kuwa Meya wa jimbo la Allar.


Mnamo tarehe 02 Mei 2013 akiwa na umri wa miaka 14 (Miaka 15 kasoro miezi mitatu), Bashaer Othman alichaguliwa na wananchi wake kuongoza jimbo lenye wakazi zaidi ya 9000 kama Mstahiki Meya wa Allar kwa kipindi cha miaka 5 akiwa na kauli mbiu isemayo "Nothing Is Impossible". Malengo yake ilikuwa ni kuwaweka vijana wote wa kiPalestina katika agenda za kisiasa ndani ya  mamlaka ya Palestina.
Ndani ya miezi 3 tu, kutokana na ufanisi mzuri wa kazi, Bashaer Othman aliteuliwa na Rais wa Mamlaka ya Palestina Bw. Mahmoud Abbas kuwa Waziri wa Utawala wa Ndani (Local Administration) katika siku ambayo alikuwa akisherehekea siku yake ya kuzaliwa akitimiza miaka 15 kamili mnamo tarehe 17 Agosti 2013. 

Uteuzi huu ulimfanya kuweka rekodi ya kuwa Waziri mwenye umri mdogo kuwahi kutokea duniani mpaka sasa na pia kuwa Meya wa kwanza wa kike kuongoza jimbo lenye wakazi zaidi ya 9000. Katika kuapishwa kwake, Waziri Mkuu wa Palestina (kabla hajajiuzuru) ndugu Salam Fayyad aliweza kusema "She could have spent the long hot summer holiday hanging out with friends or helping at home, but instead she's making speeches, signing documents, chairing meetings, attending civic functions and meeting citizens as Mayor of Allar"  akimaanisha kuwa, Huyu binti ilitakiwa atumie muda wake kufurahi na marafiki zake au kusaidia shughuli za nyumbani ila alitumia muda wake katika kuhutubia, kusaini nyaraka mbalimbali, kuongoza na kusimamia vikao, kujihusisha na shughuri za kiraia na kukutana na wananchi wa jimbo lake akiwa kama Meya wa Allar.
 
Katika nafasi yake ya Uwaziri, tayari ameanzisha mikakati mbalimbali ya kuwainua vijana nchini Palestina ikihusiana na kutoa nafasi kwa vijana kushiriki kwenye shughuli za kijamii pamoja na kuwa sehemu muhimu katika mfumo wa kisiasa wa Palestina kwa siku zijazo. Katika uongozi wake pia, Dada huyu Mheshimiwa ameweza kuwahimiza wanawake wengi zaidi nchini humo kujituma na kujiingiza katika shughuri za kiuchumi na kisiasa pia.
Binti huyu alinukuliwa akisema "At the begining, people were criticised because of our age, but then they saw us working, and that we were tough and dedicated, and now they respect us" akiwa na maana ya kwamba, wakati anaanza majukumu yake, watu walimdharau na kumkosoa sana kwa sababu ya umri mdogo alionao, ila wameona anafanya kazi kwa nguvu na kutoa mfano katika jamii sasa wanamheshimu. Vilevile binti huyu anasema anatamani kutengeneza miradi mingi itakayotoa fursa za ajira kwa vijana ili kuwazuia vijana wengi wa kiPalestina wanaotimkia nchini Israel kufanya kazi za kujitolea. " Many people are crossing the Green Link to work, instead of them going to work as Cheap Labours in Israel, we need to create jobs here".

Pamoja na muda mchache wa kuwa kiongozi mkubwa nchini Palestina, Bashaer anatumiwa na nchi yake katika ufanyaji wa maamuzi na pia kuwainua vijana ambapo ameunda Tume ya Vijana wenye upeo mkubwa na uweredi wa kutengeneza sera bila kuzingatia utofauti wa vyama vya kisiasa uliopo nchini umo ili kutengeneza uzito wa kisiasa na elimu bora kwa kizazi cha sasa na kijacho nchini Palestina.
Pia ameweza kuhudhuria vikao kadhaa vya Umoja wa Mataifa vinavyohusu mgogoro wa ardhi uliopo kati ya Palestina na Israel.

Huyu ndio Bashaer Othman, Waziri mwenye rekodi ya umri mdogo kuliko wote Duniani na pia mwenye kipaji cha hali juu katika uongozi.

           Imeandaliwa na..............
                                                   Harvey Steven

0 comments:

Post a Comment