Facebook

Tuesday, 21 October 2014

Manchester United yabanwa mbavu Ligi Kuu Uingereza.

 

Ligi kuu ya England imeendelea jana usiku ambapo Manchester United ilijikuta ikibanwa mbavu na kushindwa kufurukuta ugenini kwa West Bromwich Albion na kutoka sare ya mabao 2-2 licha kwamba ilitawala mchezo huo.

Mchezo huo wa pekee kwa ratiba ya ligi hiyo ulishuhudiwa Man United ikishindwa kupata walau ushindi wake wa kwanza nje ya uwanja wake wa nyumbani tangu timu hiyo iwe chini ya kocha Louis Van Gaal.

Ni bao la Daley Blind katika dakika za mwisho za mchezo ambalo limeiokoa Manchester United kuzama katika mpambano huo. 

Awali Stephane Sessegnon wa Westbrom aliitungua United kwa bao la mapema kabla ya Marouane Fellaini aliyeingia kipindi cha pili kusawazisha muda mfupi tu baada ya kuingia uwanjani.
Mshambuliaji kijana Saido Berahino aliipatia Westbrom goli la pili ambalo lilidumu hadi pale Blind aliposawazisha na kuinusuru United na kichapo katika mtanange huo uliochezeshwa na mwamuzi Mike Dean.

Related Posts:

  • Daley Blind "Siko tayari kulinganishwa na Roy Keane"  Blind alisema ameyazoea maisha ya Manchester United kwa muda mfupi,lakini asisitiza kuwa nimapema sana kumlinganisha na Roy Kean, Blind alisema "tusiende mbali sana,maendeleo yangu ni mazuri kwa sasa lakini ndo kwanz… Read More
  • Ronaldo kuzeekea Real Madrid   Cristiano Ronaldo hana nia ya kurejea Manchester United na atamalizia kucheza soka yake Real Madrid, amedai wakala wake Jorge Mandes.  Ronaldo, 29, tayari amefunga magoli 15 msimu huu, ikiwemo kufikisha … Read More
  • MANCHESTER UNITED WAPO TAYARI KUMLIPA TYLER BLACKETT £ 50,000 KWA WIKI-Uongozi wa Manchester United umetangaza rasmi kwamba wapo katika hatua ya mwisho ya kuuboresha mkataba wa beki kinda mwenye umri wa miaka 20,Tyler Blackett ili aendelee kuwepo kikosini hapo baada ya kuonekana bora na kocha V… Read More
  • John Stones nje hadi 2015 Beki wa Everton na timu ya taifa ya England John Stones huenda asicheze hadi mwakani baada ya kuthibitishwa kuwa anahitaji kufanyiwa upasuaji katika kifundo cha mguu. Stones, 20, aliumia katika mchezo dhidi ya Mancheste… Read More
  • MATOKEO YA MECHI ZA KUFUZU EURO 2016 Group C Slovakia (Kucka '17, Stoch '87) 2-1 Spain (Alcacer 83) Belarus 0-2 Ukraine (Martynovich '82 og, Sydorchuk '90) Macedonia (Trajkovski '20, Jahovic '66,Abdurahimi '90) 3-2 Luxembourg (Bensi '39, Turpel '44) Group E Engl… Read More

0 comments:

Post a Comment