Facebook

Tuesday 21 October 2014

Msanii Y.P wa kundi la TMK Wanaume Family afariki dunia.

MENEJA wa kundi la TMK Wanaume Family aliye pia
mkurugenzi wa MKubwa na Wanae, Said Fella
'Mkubwa' amethibitisha kuwa msanii YP amefariki
dunia usiku wa kumakia leo.
Akizungumza na BantuTz  hivi punde kwa njia ya simu, Fella
alisema YP amefariki akiwa katika Hospitali ya Temeke na siyo nyumbani kwao kama taarifa za
awali zilizokuwa zimetufikia na kwamba alikuwa
akisumbuliwa na maradhi ya Kifua.
'Ni kweli YP amefariki akiwa Temeke Hospitali
alikokuwa amelazwa kwa siku kadhaa, alikuwa
akisumbuliwa na Kifua, kwa kweli ni pigo kwetu na tasnia nzima ya muziki kwani ni hivi karibuni
tumetoka kumpoteza pia Side Mnyamwezi,"
alisema Fella mmoja wa wadu wa muziki
waliosaidia kukuza muziki wa kizazi kipya kwa
kuibua vipaji kila uchao.
Fella alisema kwa sasa wanasubiri kuwasiliana na ndugu na familia ya marehemu YP kwa ajili ya
kujua mazishi yake yatafanyika lini na wapi, japo
alisema huenda akazikwa leo pande za TMK.
Mwenyezi Mungu Ailaze Roho ya Marehemu Mahali
Pema Peponi.

0 comments:

Post a Comment