Facebook

Friday 3 October 2014

Linex akamatwa na wanajeshi,kisha kavuliwa Nguo.

  Linex


Kitu kama hiki kiliwahi kumtokea mwana-hiphop Young Killer miezi michache iliyopita ambapo alivuliwa nguo ya jeshi aliyokua ameivaa.Wiki kadhaa baadae ikatangazwa tena kwenye vyombo vya habari kwamba ni marufuku kwa watu wasio Wanajeshi kuvaa nguo hizo.
Jana yamemkuta Linex baada ya kukamatwa na wanajeshi akiwa amevaa nguo za Jeshi,hiki ndicho alichokisema baada ya kukamatwa
  ‘Sikutaka kuwa mtata jamaa walikuja wakasema ile ni nguo yao nikaingia kwenye gari iliyokua imenipeleka Airport pale nikavua nikawapa sababu lazima niliheshimu jeshi la nchi yangu‘

nguo za jeshi  
‘nilikua nimevaa kama zinataka kufanana na nguo za jeshi, zinataka kufanana kwa mbali lakini sio nguo ya jeshi‘
"Big up kwa Wanajeshi waliofanya vile labda mimi ndio nilitakiwa kuwa mfano kwa watu wengine wanaozivaa mtaani, kwa ushauri tu ni kwamba Wanajeshi wapite kwenye maduka pia yanayouza nguo zinazofanana na nguo zao wachukue’ – Linex


0 comments:

Post a Comment