Facebook

Saturday 25 October 2014

Diego Costa hatihati.


Diego Costa huenda akacheza katika mechi ya
Ligi Kuu ya England dhidi ya Manchester United
licha ya kuugua na kulazimika kupelekwa
hospitali.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Spain,
26, amekuwa akipata nafuu akiwa nyumbani na
kutakiwa kufanya mazoezi peke yake kutokana
na ugonjwa huo. Hata hivyo kwa mujibu wa
meneja Jose Mourinho, mshambuliaji huyo ana
uwezekano wa kucheza Old Trafford siku ya
Jumapili. "kila kitu kimemtokea," amesema
Mourinho. "Lakini ana nafasi ndogo ya kucheza.
Tunajaribu." Huku Loic Remy akiwa majeruhi
kutokana na jeraha la nyonga, Chelsea watahitaji
sana kuwa na Costa aliyenunuliwa kwa pauni
milioni 32.

0 comments:

Post a Comment