Facebook

Saturday 4 October 2014

Joel Harlow "Ukistajaabu ya Musa Utayaona ya Firauni"


Duniani kuna binadamu wengi sana,lakini kila bila binadamu hupewa kipawa chake,wengi wetu tunaamini Mungu humpatia kila binadamu kipawa chake,Kuna baadhi ya binadamu wanaweza kuwa na vipawa lakini wasiweze kuvitambua vipawa vyao kutoka na sababu mbalimbali.Sababu kubwa ambao naiona huwa ni mazingira tunayoishi na kujitambua,kwani unaweza kuishi sehemu ambayo jamii hiyo haikitambui na kukipa nafasi kipawa chako kiweze kufanya jambo lolote katika jamii.Hatimaye unaweza kuishi hadi mauti yakakukuta haujatumia hata theluthi ya kipawa chako.
Lakini kwa namna moja au nyingine kipawa kinaendana na bahati,mfano mzuri Christiano Ronaldo alipata nafasi ya kwenda kuchezea Sporting Lisbon na kisha kununuliwa na Manchester United na leo hii anachezea Real Madrid kutokana na kipawa chake kiliochoambatana na bahati,Kwa sababu "Nyuma ya kapeti" ni kwamba rafiki yake wa Christiano Ronaldo ndiye alitakiwa kuchukiliwa na klabu ya Sporting Lisbon lakini rafiki yake aliona ni bora aende Ronaldo.
Binadamu wengine kama Isaac Newton,Leonardo Da Vinci,Mark Zuckerberg,Steve Jobs na wengine wengi waliweza kuvitambua na kutumia vizuri vipawa vyao wakafanya makubwa duniani,kila binadamu akawa anajiuliza imewezekana vipi.Lakini jibu linabaki palepale kujitambua na kukitumia kipawa chako ipasavyo na kuwa katika mazingira yanayohitaji kipawa chako.

Leo hii katika "Jicho Langu La Tatu" namuangazia binadamu mwingine ambaye wengi wetu hatumfahamu lakini tunafahamu na kuzitambua vizuri sana kazi zake mbalimbali kutokana na kipawa kikubwa alichonacho.
Anaitwa Joel Harlow aliyezaliwa miaka 45 iliyopita huko Grand Forks, North Dakota-Marekani.
Joel Harlow ana kipawa kikubwa sana cha kubuni na kutengeneza "zombie" na "katuni".Alipokuwa mdogo alivutiwa sana na sinema ya KING KONG aliyoandaliwa mwaka 1933,alipenda sana jinsi sinema hiyo ilivyotengeneza,aliweka nia na malengo hapo baadae na yeye atengeneza sinema kama hizo.
Alipotimiza umri wa kusoma "College" aliamua kwenda katika Jiji moja kubwa linalopatikana huko Marekani liitwalo New York.Alisomea masomo ya "Animation and Designing" katika Chuo cha Visual Arts lakini yeye binafsi alipenda zaidi kusomea masuala ya "Special makeup Effects".Hapo ndipo ninapojifunza kwamba Joel Harrow alikitambua kipawa,kwani kutokana na mazingira yaliyombana kule Grand Forks aliamini asingeweza kutimiza ndoto zake na kukitumia kipawa chake ipasavyo akaamua kuhamia New York.Lakini Joel Harlow alipokuwa anasoma katika Chuo hicho alipata uzoefu mkubwa na alifanikiwa kuwa miongoni mwa waliotengeneza sinema mbili za kutisha “The Toxic Avenger” (parts II and III) na “Basket Case 2".

 Baadae Harlow alihamia Magharibi mwa Jiji la Los Angeles,ambapo ndoto zake na kipawa chake kilienda kuvumbuliwa rasmi na kutumika ipasavyo kwani alikwenda kujifunza huku akifanya kazi katika Chuo cha "Special makeup Effects" vitu ambavyo anavipenda Joel Harlow,na alipohitimu akaajiriwa katika kampuni ya XFC Inc ambayo ilikuwa chini ya Steve Johnson,alifanya kazi kwa kujituma na juhudi kubwa huku akiwa ametengeneza sinema mbalimbali takribani miaka nane yeye akiwa upande wa utengenezaji wa Binadamu ambao wanabadilishwa na kuwa "wafu walio hai" yaani "zombie".


Kwa ustadi mkubwa Joel Harlow akionekana kuwa na ubunifu na akili nyingi sana katika kitenge cha "Special Makeup Effects" alifanikiwa kuwa katika jopo la waliotengeza sinema kama “How the Grinch Stole Christmas,” “A.I. Artificial Intelligence,” “Planet of the Apes,” “Constantine” na “Pirates of the Caribbean: The Curse of the Black Pearl,” huku akiwa ametengeneza uhusiano mkubwa na uliojengeka vizuri kutokana na misingi ya kazi zao na waongozaji "directors" wakubwa wa sinema kwa kipindi hicho,Director Gore Verbinski,Johnny Depp na muandaaji "Producer" Jerry Bruckheimer. vile vile alihusika katika utengenezaji wa sinema nyingine zilizofuata Dead Man’s Chest” na “Pirates of the Caribbean: At World’s End.

Kutokana na kazi nzuri alizozifanya mwaka 2010 aliweza kushinda tuzo ya "Star Trek" kupitia sinema ya JJ Abrahams,mwaka huo huo akashinda tena tuzo ya "Critic’s Choice award" kupitia sinema ya Alice in Wonderland" "Pirates of the Carribean.

Ukiachana na sinema hizo,Harlow ametengeneza binadamu/waigizaji aliowageuza "Zombie" kupitia sinema kama  “Dark Shadows” “Buffy the Vampire Slayer” "The Lone Ranger (2013 film)"


The Lone Ranger (2013 film)
Ukiachana na ustadi na kipawa kikubwa alichonacho katika utengenezaji wa "zombie".Hivi sasa Joel Harlow amefungua kampuni yake yeye mwenyewe iitwayo Joel Harlow Designs ikiwa inajihusisha na masuala ya utengenezaji wa "zombie", na binadamu kutisha kupitia maabara yake kubwa aliyoijenga huko New York-Marekani.



Lakini kikubwa na cha kuvutia zaidi ni Utengenezaji wa SAMAKI MTU ajulikanaye kama "NGUVA" lakini kwa ile lugha ya kimombo anajulikana kama "MERMAID".Nadhani watu wengi wanakumbuka ile taarifa iliyoripotiwa katika vyombo mbalimbali vya habari hususani mitandao ya kijamii kuwa samaki aina ya "nguva" au "Mermaid" amepatikana akiwa amekufa katika fukwe za bahari huko Berlin-Ujerumani baada ya kula kitu chenye sumu na wengi wetu tuliamini kuwa tukio lile ni kweli,lakini ukweli ni kwamba yule hakuwa "nguva" halisi bali ilikuwa ni kazi ya Joel Harlow.

Najua inaleta mkanganyiko sana katika kuamini jambo hili kwani hata madaktari bingwa walioenda kumchunguza samaki "Nguva" aliyekutwa amekufa katika fukwe huko Berlini walisema amekufa kutikana kula chakula chenye sumu,lakini ukweli ni kwamba hicho ndicho kipawa alichonacho Joel Harlow ambaye alikigundua mapema na kuanza kufanya kila liwezekanalo aweze kukitumia vyema. Na nguva yule aliyekutwa amekufa,kifo chake kilisababishwa na mashine kushindwa kufanya kazi kwani mashine ile ilitengenezwa kumuwezesha "Nguva" huyo kuishi kwa muda wa mwezi mmoja.

ANGALIA HAPA VIDEO YA UTENGENEZAJI WA NGUVA ALIYEKUTWA AMEKUFA HUKO BERLINI-NGUVA ALIYETENGENEZWA NA JOEL HARLOW
Mermaid bodies by Joel Harlow for Pirates of the Caribbean On Stranger Tides (photo Michael Spatola)
Joel Harlow kupitia kampuni yake waliweza kumtengezaa samaki huyo na kisha kumuwekea mashine iliyomuwezesha kupumua kama samaki "Nguva" halisi,alimtengeneza samaki huyo kwa kutumia vitu mbalimbali kama samaki huyo anavyokuwa kwa muda usiopingua mwezi mmoja na kisha kumuweka majini.

Hilo halikuwa sio tukio la kwanza la Joel Harlow kwani amekuwa akitengeneza binadamu wafu "Zombie" na kisha kuwapandikiza katika msitu mmoja mkubwa uliopo Marekani..Hakika ukistajaanu ya Musa Utayaona ya Firauni.Inasemekana msitu huo hivi sasa una "zombie" wa kila aina na unatisha kwelikweli


ANGALIA HAPA ZA VIDEO ZA VIUMBE MBALIMBALI VINAVYOTENGEZWA NA JOEL HARLOW
                              -Bantu Video 1
                              -Bantu Video 2


Huyo ndiye Joel Harlow aliyekitendea vyema kipawa alichopewa na mwenyezi Mungu,ni binadamu wachache sana wanaoweza kufanya maajabu kama ya bwana Joel Harlow,katika dunia ya sasa ukiona sinema yenye "Zombie" wa kutisha basi kaa ukijua itakuwa ni kazi ya Joel Harlow kwani hivi sasa yeye ndiye anayepewa tenda zote na "Hollywood" katika utengenezaji wa "Zombie",vilevile ameingia mikataba na makampuni makubwa ya utengenezaji wa filamu na sinema mbalimbali nchini Marekani,ameingia mikataba na kampuni kama Fox Cinema,21st Century Cinema,GMG Cinema,WWE Cinema,CMC Cinema,Golden Pictures Cinema,AK Fil Production na nyingine nyingi.


Natumai umejifunza kitu kutoka kwa Joel Harlow.Endelea kutembelea www.bantutz.com huku ukisubiri kwa hamu ujio wa Mtandao mpya wa kijamii kutoka BantuTz Entertainment kwani nitakuwa na sehemu yangu maalumu kwa ajili ya makala hizi za "JICHO LANGU LA TATU".


Imeandaliwa na.....
                              Katemi P. Methsela
                             +255716418657
                                 +255785442107

0 comments:

Post a Comment