Facebook

Thursday 9 October 2014

Ronaldo kuzeekea Real Madrid

 Photo: Cristiano Ronaldo 'KUZEEKEA' MADRID
Cristiano Ronaldo hana nia ya kurejea Manchester United na atamalizia kucheza soka yake Real Madrid, amedai wakala wake Jorge Mandes. Ronaldo, 29, tayari amefunga magoli 15 msimu huu, ikiwemo kufikisha hat trick 22 katika La Liga. Taarifa zimekuwa zikimhusisha Ronaldo kurejea Old Trafford kwa uhamisho wa pauni milioni 80. Mendes amesema: "Cristiano ameridhika sana Real Madrid. Ataendelea kuvunja rekodi zote hapo na kustaafu hapo." Wakala huyo amekiambia kituo cha radio cha Cadena COPE kuwa: "Huwezi kupata mchezaji mwingine kama yeye. 
"Anaendelea kuwa mchezaji bora, na ataendelea kuwa hivyo hadi atakapofika umri wa miaka 40.
"Anaipenda United kwa sababu moyo wake ulikuwa pale kwa miaka sita. Lakini sasa vyote anavyofikiria ni Real Madrid na atakuwepo hapo.
"Ndoto ya Cristiano ni kushinda Champions League. Huwa bado ana njaa, na siku zote anataka zaidi.
"Haishi kushangaza watu. Ni vigumu kupata mtu yeyote kama yeye katika historia ya soka."
Ronaldo aliondoka Manchester United kwenda Real Madrid mwaka 2009 kwa uhamisho wa pauni milioni 80.
Meneja wa Manchester United Louis van Gaal alikiri mwezi uliopita kuwa angependa kumsajili kiungo huyo, lakini hatarajii kama Real Madrid watakuwa tayari kumuuza.

Cristiano Ronaldo hana nia ya kurejea Manchester United na atamalizia kucheza soka yake Real Madrid, amedai wakala wake Jorge Mandes. 
Ronaldo, 29, tayari amefunga magoli 15 msimu huu, ikiwemo kufikisha hat trick 22 katika La Liga. Taarifa zimekuwa zikimhusisha Ronaldo kurejea Old Trafford kwa uhamisho wa pauni milioni 80. 
 
Mendes amesema: "Cristiano ameridhika sana Real Madrid. Ataendelea kuvunja rekodi zote hapo na kustaafu hapo." 
 
 Wakala huyo amekiambia kituo cha radio cha Cadena COPE kuwa: "Huwezi kupata mchezaji mwingine kama yeye.
"Anaendelea kuwa mchezaji bora, na ataendelea kuwa hivyo hadi atakapofika umri wa miaka 40.
"Anaipenda United kwa sababu moyo wake ulikuwa pale kwa miaka sita. Lakini sasa vyote anavyofikiria ni Real Madrid na atakuwepo hapo.
"Ndoto ya Cristiano ni kushinda Champions League. Huwa bado ana njaa, na siku zote anataka zaidi.
"Haishi kushangaza watu. Ni vigumu kupata mtu yeyote kama yeye katika historia ya soka."
 
Ronaldo aliondoka Manchester United kwenda Real Madrid mwaka 2009 kwa uhamisho wa pauni milioni 80.
Meneja wa Manchester United Louis van Gaal alikiri mwezi uliopita kuwa angependa kumsajili kiungo huyo, lakini hatarajii kama Real Madrid watakuwa tayari kumuuza.

0 comments:

Post a Comment