Facebook

Tuesday 14 October 2014

"SIKU YA WANAFIKI KUMDHIHAKI BABA WA TAIFA Mwl J.K NYERERE"



Leo ni siku ya wanafiki kumdhihaki Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere,ni siku ya wanafiki kuwadhihaki watanzania.Njia pekee ya Kumuenzi Mwalimu ni kuyaishi matendo yale mema aliyolitendea taifa hili.
Leo mafisadi ndio wanaotunga na kuandika sheria mama ya nchi(Katiba) na kupuuza maoni ya wananchi.Haitakubalika hata kidogo.


Leo mafisadi na watawala waliovimbiwa makombo mezani pa mafisadi ndio wanaoimba nyimbo za sifa na tenzi laini kuwa wanamuenzi baba wa Taifa.

Leo hii wazalendo wanaopigania raslimali za taifa hili wanaonekana maadui na taifa linakubali na kuwaacha wapweke.


 
Leo hii akina David Kafulila wanaitwa Tumbili na mawakala wa ufisadi waliovishwa vilemba na majoho ya kitaaluma na kiutawala eti kwa kuwa wamewaanika mabwana zao.Sisi vijana tumekaa kimya .
 
Tumeona wasomi na wanaharakati na hata baadhi ya wanahabari wakizibwa midomo .Mafisadi kwa kushirikiana na watawala wameamua kutumia mahakama kutisha wazalendo.

Serikali imewekwa mifukoni mwa mafisadi.

Taifa linadhalilishwa sisi tukiwa kimya huku tukimdhihaki baba wa taifa aliyechukua hatua kali dhidi ya fisadi wa kigiriki aliyedai kuwa ameiweka serikali yake mfukoni mwake.

Kitendo cha Mwalimu Nyerere kumkamata na kumuweka gerezani ni kinyume kabisa na hali ya sasa ambayo wanaotamba kuiweka serikali mfukoni wanathibitisha kwa kutumia mahakama kutishia wazalendo huku wakisaidiwa na watawala .


Matusi ya Mwanasheria Mkuu na pia katibu Mkuu wa Wizara Eliakim Maswi ni dhihaka na uthibitisho wa serikali kuwekwa mfukoni.

Sasa kwa kulinda hadhi na heshima ya taifa hili,kwa kulinda raslimali za nchi hii zinazotumika na wachache huku mamilioni ya watanzania wakikosa huduma muhimu kama ajira,elimu huku vifo vya akina mama na watoto vikishamiri.Watanzania wenzetu hawa wanavumilia kuwa watanzania wakati watawala na mafisadi wakijivunia kuwaibia watanzania.Sasa tumeamua kumuenzi Mwalimu Nyerere kwa kuchukua hatua .Kesi aliyofunguliwa Kijana David Kafulila ni kesi ya vitisho yenye lengo la kuhalalisha ufisadi na uporaji wa raslimali za nchi hii .Hatutakubali.


Nitaratibu kuhakikisha wale wote wenye misimamo mikali ambao wako tayari kuunganishwa kwenye kesi hii tunaungana na Kafulila na wanaharakati wengine zaidi ya 100 walioomba kuunganishwa kwenye kesi hii hadi sasa .Kesi ilifunguliwa na IPTL baada ya Kafulila kuibua kashfa ya wizi wa Sh.Billioni 200 kutoka Akaunti ya Escrow .


Ana nyaraka zote muhimu na amenihakikishia kuwa atatoa ushirikiano wote.Ni lazima tuwe na "solidarity" katika kuchukua hatua hizi za kiuanamapinduzi.Hizi ni harakati za kuiondoa serikali mfukoni mwa mafisadi.

Taifa haliwezi kudhalilishwa huku vijana ,akina mama na wazee ,wasomi ,wakulima,wafanyabiashara waadilifu wanaonyanyaswa kila siku kulipa kodi hata kwa dhuluma wakiendelea kukaa kimya.Kama upo tayari kuingia katika mapambano haya tafadhali nitumie Majina yako kamili na sehemu unayoishi haraka kupitia namba 0768078523.Hatuingilii uhuru wa mahakama bali tunataka kuingia mahakamani .

Tukishakamilisha Zoezi hili tutafuata hatua nyingine itakayotoa fundisho kwa utawala huu.

Rais Kikwete na Serikali yake wajiandae sasa.Wanajihesabia wamebakiza mwaka 1 kumaliza awamu yao madarakani lakini huo Mwaka Mmoja unaweza usitimie wakafika ukingoni siku za karibuni.Demokrasia inaruhusu,sio haramu 



Jana BantuTz waliripoti taarifa hii...........
"Kundi la wafadhili 12 wa kimataifa limechelewesha msaada wao katika bajeti ya Tanzania hadi matokeo ya uchunguzi juu ya madai ya rushwa katika sekta ya nishati yatolewe, na hatua stahiki zichukuliwe."

Tutajiandaa na kukutana kwenye Ukumbi maalumu weekend hii kwa ajili ya kujipanga kikamilifu katika vita hii.

Tumeanzisha kampeni "Bring back our Money" au "Rudisha Pesa Zetu"

Tutachukua hatua kali ya kihistoria .

It's a National Salvation Movement.We shall fight bravely against Lootocracy(Looting) .

Tumuenzi Mwalimu Nyerere kwa kuiondoa Serikali yenye Amri Jeshi Mkuu mifukoni mwa mafisadi.

Aluta Continua,Victory Ascerta.....

"Pumzika Kwa Amani Mwl.J.K Nyerere.Mungu Ibariki Tanzania,Mungu Ibariki Afrika"  


Imeandaliwa na.........
                                  Ben Saanane
                                  @ Ben saa8

0 comments:

Post a Comment