Facebook

Wednesday 25 February 2015

Mtanzani afurahia kufungwa kwa meneja wake kisa ya usafirishaji wa madawa ya kulevya Japan.

Msanii wa muziki Iryn Namubiru ambaye mwezi Mei mwaka 2013 alikamatwa na dawa za kulevya huko Japan, hatimaye ametuliza moyo wake baada ya mtuhumiwa anayedaiwa kumbambikiza dawa hizo, Ueno Kim kuhukumiwa miaka 13 jela na faini ya shilingi milioni 14.

Iryn amesema kuwa, hajisikii huruma yoyote kwa Ueno ambaye alikuwa meneja wake kutokana na kitendo alichomfanyia kumharibia maisha yake, akitaka sheria kuchukua nafasi yake na kuhakikisha kuwa anaozea gerezani.
Kesi hiyo ya usafirishaji wa dawa za kulevya imemalizika huko Japan na kuacha katika rekodi ya Iryn historia ya kuwekwa kizuizini kwa muda kabla ya ukweli halisi kuja kufahamika

0 comments:

Post a Comment