Facebook

Tuesday 24 February 2015

UCHAMBUZI MECHI ZA LEO LIGI YA MABINGWA BARANI ULAYA NA Mr.CHOI {KWA TAARIFA YAKO}

 

===================================================
Manchester City VS Barcelona   22:45
M.Pellegrini Vs Luis Enrique

                

        Baada ya Chelsea,PSG,Shaktar,Bayern kutoa sare michezo yao huku Real Madrid wakiwafunga Schalke 04 wiki hii kipute cha Uefa kinaendelea na siku ya leo hizo mechi ndio zinahusika.
     Pale katika dimba la Etihad Man City watapambana na Barcelona katika mchezo kama huu tulishuhudia Man city wakitolewa mashindanoni  kwa jumla ya goli 4-1 huku Martin Demichelis akitolewa kwa kadi nyekundu pale Etihad kwa kumchezea rafu Messi.

    Licha ya kufungwa na Malaga katika mchezo wa ligi huku Man City wakiwafunga N'castle 5-0 bado mchezo utakuwa mgumu kwa pande zote kutokana na ubora wa vikosi pia rekodi zao katika michuano hii.
     Man City watahitaji kuandika historia nyingine ya kuendelea hadi robo fainali huku Barca wakihitaji tunza heshima yao mbele ya Man City na katika hatua hii.


   Suarez ndani ya Etihad baada ya kuondoka Liverpool leo anatua katika ardhi ya England akiwa na jezi za Barca huku upande mwingine Bonny kwa mara ya kwanza kucheza Uefa akiwa na jezi za Man City.
   Man City ni miongoni mwa timu zenye safu nzuri ya ulinzi na kiungo hasa kutokana na nguvu za maumbile makubwa ya wachezaji wao ingawa wasipo kuwa makini yanaweza kuwa sumu kutokana na uchezaji wa Barca lakini wakiwa makini kwa uzito wa kikosi chao haitokuwa kazi kuwafunga Barcelona
   Barca wao katika safu ya Ulinzi bado imekuwa ni tatizo na leo wasipo kuwa makini safu ya mashambulizi ya Man City ikiongozwa na Aguero itawapa tabu sana ila kwa upande wa kiungo amna tatizo na ukija safu ya ushambuliaji hupaswi kuwa na hofu kutokana na ubora wake ikiongozwa na Messi ambaye tangu mwaka uanze ndo mchezaji mwenye magoli mengi barani Ulaya akifuatiwa na Kane.
    Barca bado watamkosa Thomas Vermaelen lakini kwa vikosi vya kwanza kwa timu zote hakuna majeruhi.
   Ngoja tusubiri ni kina Aguero,Silva,Bony au ni MSN international kombinenga.

NB::Katika michezo 13 ya mechi za nyumbani  Champions League Man city haikuruhusu goli katika mchezo mmoja tu ilikuwa dhidi ya B.Munich mwezi wa 12/2011 na matokeo yalikuwa 2-0 .
   - Hivi karibuni Katika mechi saba zilizopita dhidi ya timu za England ,Barcelona wamepoteza mchezo mmoja tu na ilikuwa dhidi ya Chelsea nusu fainal 2011/2012 ambapo walitolewa kwa jumla ya goli 3-2 matokeo ya jumla.

----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

 JUVENTUS vs B.DORTMUND 22:45
     M.Allegri VS Jürgen Klopp

Ukiachilia mbali mchezo wa Man City  dhidi Barca kipute kingine kitakuwa pale Juventus stadium.
    Dortmund wamekuwa wakifanya vyema katika Uefa tofauti na katika ligi yao mchezo huu watakuwa na hamasa hasa baada ya kushinda michezo mitatu mfululizo ya ligi ikichagizwa na kiwango bora cha Pierre-Emerick Aubameyang’s na Reus .


    Juventus wakiwa vinara wa serie A huku hawajapoteza mchezo tangu Mwezi wa kumi walipo fungwa na Genoa ni timu pekee kutoka Italy katika hatua hii ya 16 bora ni miongoni mwa vikosi bora hasa katika safu ya kiungo inayo ongozwa na kina Pogba,Pirlo na Vidal ambaye leo atarejea uwanjani.
   Klopp anamatumaini rik Durm, Jakub laszczykowski, Mats Hummels na Jeremy Dudziak kucheza leo baada ya majeraha kadhaa kuwakabili upande wa Juve hakuna tatizo.
    Katika mchezo wa leo timu hizi zina utofauti Juve ni wazuri sana katika safu ya ulinzi na kiungo huku Dortmund wakiwa wazuri sana katika safu ya ushambuliaji

NB:: Dortmund walichukua ubingwa wa Uefa champions league 28 May 1997 kwa kuifunga Juventus goli 3-1 fainali ilifanyika pale Ujerumani wafungaji kwa Dortmund walikuwa Karl-Heinz Riedle  aliye funga mawili na Lars Ricken huku upande wa Juve ni mfalme Del piero.

    - Juve wameshinda mara 14 dhidi ya timu za Ujerumani katika uwanja wa nyumbani wakitoa sare mara mbili na kupoteza mara tano.
  - Dortmund wameshinda mara nne kati ya 14 walizocheza na timu za  Italy mara ya mwisho ni msimu wa   2008/9.


 -----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
Endelea kutembelea www.bantutz.com kwa uchambuzi makini katika masuala mbalimbali hususan michezo.
---------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

 Imeandaliwa na................
                                               CHOIKANGA
                                             Choikangta.ckt@gmail.com
                                               WhatsApp -0765 691418

----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

0 comments:

Post a Comment