Facebook

Sunday 22 February 2015

Uchambuzi wa michezo ya jana Ligi Kuu Uingereza na Mr Martin Kiyumbi.

 Santi Cazorla celebrates after scoring a penalty against Crystal Palace
Jana Ligi Kuu Uingereza iliendelea imeanza huku michezo mbalimbali ilipigwa katika viwanja mbalimbali.Hebu tujaribu kuangalia vitu vichache vilivyotokea kwenye michezo ya jana.


Swansea City 2-1 Manchester United 

 Mchezo huu uliisha kwa swansea city kumfunga Man United.Hii inamaanisha Swansea msimu huu amemfunga Man United mara mbili.Hii ni mara ya kwanza katika historia Swansea kuifunga Man United nyumbani na ugenini.
Jana United hawakuwa na bahati .Mchezo kipindi cha kwanza ulikuwa sawa.Kipindi cha pili United walimiliki mchezo ila bahati haikuwa kwao kama Van Gaal alivyosema baada ya mchezo.
Walikuwa wamelijaribu lango la Swansea City mara18 goal lakini zilizokuwa mshuti yaliyolenga goli ni 3 tu.

Rooney jana alilenga goli kwa mara ya kwanza kwa mwaka  2015.Ander herrera amefunga goli kwenye michezo mitatu aliyoanzishwa.Mchezaji wa Swansea City Ki jana alifunga goli lake la tano msimu huu


Manchester City 5-0 Newcastle United

Man City jana iliiibuka na ushindi wa goli 5 huu ni ushindi muhimu kuliko ushindi wa mechi iliyopita dhid ya Stoke City kwasababu ushindi huu umeifanya City kupunguza pengo la pointi mpaka kubakia 5.
Pia ushindi huu unapandisha morali kueleka mchezo wao dhid ya Barcelona katikati ya juma hili.
Man City walifanikiwa kufunga magoli 3 kwa dakika 2,Sergio Kun Aguero alifunga goli lake la 17 na kumfanya mchezaji anayehusika zaidi kwa upatikanaji wa magoli msimu huu kuliko mchezaji yeyote.Aamefunga magoli 17 amehusika kwenye utengenezaji wa magoli 22.
Dzeko alifunga goli lake la kwanza tangia mwezi september mwaka jana.Anita jana alipata kadi katika sekunde ya 40 hvo kuwa kadi ya mapema kutoka  msimu huu.


Aston Villa 1-2 Stoke City

Jana ndo ulikuwa mchezo wa kwanza kwa kocha wa Aston villa.katika makocha wapya 10 waliowahi kuchaguliwa kuifundsha Villa ni makocha 2 tu walioshinda michezo yao ya kwanza.
jana Brad Guzan alitimiza mchezo wa 100 Ligi Kuu Uingereza.
Scott Sinclair jana alifunga goli lake la kwanza Ligi Kuu Uingereza tangia August 2012.Stoke City haijawahi kufungwa michezo mitano waliyoenda Villa Park.



Chelsea 1-1 Burnley 

Mourinho amelalamikia kadi nyekundu ya Nemanja Matic.Ila kiuhalishia kama  mchezaji wa kimataifa hakusitahili kufanya maamuzi yale bila kusubiri maamuzi ya refa.
kwa upande wangu wote wawili walistahili kadi nyekundu.Ivanovic alifunga goli la 4 katika michezo  6 iliyopita ya michuano yote. Ben Mee (R) is congratulated by team-mate Danny Ings after scoring Burnley's equaliser in the 81st minute

katika michezo 10 iliyopita Eden hazard amefunga goli 5 na kusaidia upatikanaji wa magoli 4.

Sunderland 0-0 West Bromwich Albion
Jana Adam johnson alipiga krosi 12 nyingi kwa sunderland msimu huu.Lakini mchezo huo uliisha kwa suluhu ya bila kufungana

Hull City 2-1 Queens Park Rangers
Jana Barton aliomba radhi kwa  mashabiki,wachezaji na benchi la ufundi la QPR.kwa kadi nyekundu aliyooneshwa.Amekiri wazi ilikuwa kadi nyekundu ya kipuuzi.
Jana alifikisha kadi ya 9 nyekundu.Kadi nyekundu hii ndo ikichangia kwa kiwango kikubwa QPR kupoteza.
Charlie Austin alifunga goli lake la 2 kwenye michezo 8.
katika michezo 2 iliyopita Dame N'doye amefunga goli 2 na kusaidia 2.

Crystal palace 1-2 Arsenal .
jana katika uwanja wa Selhurst park,Arsenal walizuiwa vizuri.Tumezoea kuwaona Arsenal  wakiwa wanamiliki mpira na kutengeneza nafasi nying za kufunga lakini msimu huu imekuwa tofauti hasa hasa mechi za ugenini wamekuwa wakizuia na kutengeneza nafasi chache za kuzuia na kuzitumia.

katika michezo 11waliyokutana na Crystal Palace,Arsenal imeshinda michezo 8 na kutoa suluhu tatu.
Carzola jana alifunga goli lake la 6 kwa penatli na kumfanya awe mchezaji aliyefunga goli nyingi kwa penati msimu huu.
Giroud alifikisha goli 50 la mashindano yote tangia aje Arsenal.katika michezo saba Giroud kafunga magoli 8 
kwenye michezo 5 iliyopita palace kashinda mechi moja na kutoa suluhu 3.Glen murray alifunga goli lake la kwanza tangia march 2014



Imeandaliwa na.........................
                                                    Martin kiyumbi

0 comments:

Post a Comment