Facebook

Sunday 22 February 2015

Tanzia:Aliyekuwa mchezaji nguli wa Simba Sc Christopher Alex afariki dunia.

 Displaying IMG-20150222-WA0009.jpg

Taarifa zilizotufikia BantuTz.com hivi punde kutoka mkoani Dodoma ni kwamba Mwamba umeanguka na nuru imetoeka.Ni baada ya aliyekuwa kiungo mahiri wa timu ya taifa mpira wa miguu Tanzania na vilabu vya Reli na Simba SC ya jijini Dar Es Salaam Christopher Alex Massawe amefariki dunia leo hii majira ya Saa 3:30 Asubuhi katika hospital ya Mirembe Dodoma.
Amefariki dunia baada ya kusumbuliwa na maradhi ya kifua yaliyomsumbua kwa muda mrefu.


Christopher Alex anakumbukwa zaidi mwanzoni mwa miaka ya 2000 alipokuwa anachoza soka mahiri na la kuvutia zaidi katika sehemu ya kiungo.Na kuwa miongoni mwa wachezaji bora kabisa nchini na walioiwezesha Simba SC kutandaza soka la aina yake hadi kufuka hatua za juu kabisa katika michuano ya klabu bingwa barani Afrika.

Vilevile anakumbukwa zaidi kwa penati yake ya mwisho dhidi ya Klabu ya Zamalek ya nchini Misri iliyowavua ubingwa wa Afrika miamba hao wa kaskazini mwa Afrika manmo mwaka 2003.

Ni msiba  mzito kwa wanamichezo wote nchini kwa jumla.

BWANA ALITOA BWANA ALITWAA,JINA LAKE LIHIMIDIWE. PUMZIKA KWA AMAN CHRISTOPHER ALEX MASSAWE 'MWAMBA'

0 comments:

Post a Comment