Facebook

Thursday 26 February 2015

Yaliyomtokea Ommy Dimpoz, yamkuta Chris Brown Canada.


Baada ya mwimbaji kutoka Marekani Chris Brown kuzuiliwa kuingia Canada na kusababisha kusitishwa kwa show zake mbili ambazo alitakiwa kuzifanya Canada ndani ya wiki hii.
Ommy Dimpoz ameonyesha njisi gani watanzania na mashabiki wake walilipokelea suala lake tofauti na kuonyesha kuwa watu wengi walimcheka na kumchamba wakiamini kuwa yeye ni mtu maarufu hivyo asingeweza kupatwa na suala hilo.
"Pole braza Kristofa, haya ni Mambo ya kawaida ila Mwenzio nilivyozuiwa kuingia Nchini kwenu Basi nilivyorudi kwetu nimechekwaaa,Nimechambwaa khaa,hawajuagi mambo ya Uhamiaji hawajali we nani."
Wiki ya wapendanao msanii Ommy Dimpoz alirudishwa Tanzania baada ya kuzuiwa kuingia Marekani kwa kukosa vibali vinavyomruhusu kuingia nchi hiyo kufanya show.

0 comments:

Post a Comment