Facebook

Thursday 26 February 2015

Arsenal yaambulia kipigo kikali kutoka kwa Monaco,Nyumbani.


‘Washika mtutu’ wa London timu ya Arsenal leo imepigishwa kwata na vijana wa Monaco kutoka Ufaransa kwa kuchapwa mabao 3-1 katika mchezo wa Kwanza wa hatua ya 16 bora uliopigwa katika dimba la Emirates jijini London Uingereza.
Arsenal iliyoonekana mwanafunzi wa soka kwa Monaco ambao wamewahi kufundishwa na Asern Wenger wamepigwa mabao hayo kupitia kwa Geoffrey Kondogbia dakika ya 38 na mchezaji wa zamani wa Man United Dimitar Berbatov dakika ya 53 huku bao la 3 likifungwa dakika ya 90 (Dakika za nyongeza) na Yannick Ferreira-Carrasco.
Bao la Arsenal limepatikana katika dakika ya 90 likifungwa na Alex Oxlade-Chamberlain.
Marudiano ya mechi hii ni Machi 17 nchini Ufaransa ambapo Arsenal itatakiwa kushinda zaidi ya  magoli 3-0 au 4-1.

Je kwa kuwatazama Monaco, Arsenal itaweza kuvuka hatua hii?
Arsenal imekuwa ni timu nyingine kutoka England kupoteza mchezo wa Kwanza wa hatua hii baada ya jana Man City kufungwa 2-1 na Barcelona.
Mchezo mwingine umezikutanisha Bayer Liverkusen na Atletico Madrid katika dimba la BayArena ambapo matokeo ni
Bayer Leverkusen 1 - 0 Atletico Madrid
Kwa bao la Hakan Calhanoglu dakika ya 57.
Katika mchezo huu Madrid walilazimika kucheza kupungufu kuanzia dakika ya 76 baada ya Tiago kulimwa kadi nyekundu.

0 comments:

Post a Comment