Facebook

Tuesday, 1 July 2014

Facebook yalaumiwa na watumiaji

Mtandao wa Facebook umelaumiwa kwa kuwafanyia wateja wake utafiti wa kisaikolojia bila ya kuwajulisha.
Nia ya utafiti huo ilikuwa kujua kama wateja wake wamebadili tabia ya kuweka picha na mawazo yao katika mtandao huo kutokana na kukasirishwa na tabia za baadhi ya watumiaji wenzao.
Utafiti huo uliohusisha takribani watumiaji 700,000 unaonyesha kuwa Facebook inacheza na taarifa za watumiaji wake ili kupata hisia zao katika kile wanachokiweka kwenye mtandao huo.
Hata hivyo mtandao wa Facebook umekanusha madai hayo na kwamba hakuna mtumiaji binafsi aliyelengwa na utafiti huo uliofanywa na mtandao huo kwa ushirikiano na chuo kikuu cha Cornell na California.
“Ngoja tuuite utafiti kama Facebook wenyewe wanavyouita, lakini ni dalili za wazi za kushindwa kuzingatia maadili na nguvu ya kulinda haki za watumiaji wake” amesema Kate Crawford katika ukurasa wake wa Twitter.
Waziri wa kazi Jim Sheridan mjumbe wa bodi ya mawasiliano ameagiza uchunguzi kufanyika dhidi ya mtandao huo wa Facebook katika tuhuma hizi.
Hata hivyo Katherine Sledge Moore, Profesa wa Saikolojia katika chuo cha Elmhurst , Illinois amesema kwa jinsi ambavyo Facebook wamekuwa wakishughulika na taarifa za wateja wake makubaliano yaliyopo katika utafiti huo hadhani kama yapo nje ya hali ya kawaida.
Adam Kramer kutoka Facebook mmoja kati ya walioandaa taarifa ya utafiti huo anasema wanadhani kuwa ilikuwa mhimu kwao kutafiti mashaka yanayowakumba watumiaji hasa katika mawazo yanayowekwa na marafiki zao na jinsi yanavyowafanya wafikirie tofauti .

Related Posts:

  • MAAJABU YA DUNIA:BINADAMU AGEUKA MTI Ni miujiza ya Mungu. Mitihani ipo kila kona kwa aina mbalimbali lakini hatutakiwi kukufuru. Tunapaswa kukubali matokeo na kuomba nusura kwa Muumba, kwani kazi yake haina makosa. Binadamu ageuka mti! Unaweza kudhani ni simuli… Read More
  • 10 World’s Most Beautiful National Parks National parks are naturally beautiful. Most parks were declared parks to preserve the wild beauty that makes them so amazing. While nearly all these protected areas are pretty, a number are simply amazing in their beaut… Read More
  • 20 Spectacular images of Storms. Nature is amazing; I leave here a selection of images of those that nature lovers never tire of seeing. … Read More
  • 10 Fabulous Beach Resorts in the World The world is home to some breathtaking beaches that are complemented by some of the most luxurious resorts ever created. The following resorts are situated in some of the world’s most revered vacation destinations… Read More
  • 10 Most Unusual Buildings in the World Buildings are not just structures that people live and work in.  They are pieces of art.  Architects design and engineers build extraordinary art that defy gravity, incorporate extreme creativity, and turn … Read More

0 comments:

Post a Comment