Facebook

Wednesday 30 July 2014

SINEMA ZA UHAMIAJI ZAENDELEA - Kusitishwa kwa Ajira za Konstebo na Koplo




Baadhi ya Vyombo vya Habari leo tarehe 29
Julai, 2014 vimeandika kwa makosa kuwa ajira
za Uhamiaji zilizositishwa jana zinahusiana na
70 zilizopatikana baada ya usaili uliofanyika
katika Uwanja wa Taifa.


Ukweli ni kuwa usaili wa nafasi ya Mkaguzi
Msaidizi wa Uhamiaji ambao awali ulianzia
Uwanja wa Taifa ulienda vizuri hadi
wakapatikana wasailiwa wa kujaza nafasi 70 za
Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji. Zoezi hilo
halikuwa na matatizo yoyote, na waliochaguliwa
walitakiwa kuripoti kazini tarehe 29 Julai lakini
kwa sababu ya Sikukuu sasa wataripoti baada
ya sikukuu.


Hivyo tunapenda kufafanua kuwa wasailiwa
waliochaguliwa kujaza nafasi 70 za Mkaguzi
Msaidizi wa Uhamiaji hawahusiki na usitishwaji
uliotangazwa jana na wanatakiwa kuendelea na
mipango ya kuripoti kazini kama ilivyotangazwa
hapo awali.


Wasailiwa wanaohusika na kusitishwa kwa ajira
zao ni wale waliokuwa wameshiriki katika zoezi
la kuajiri Konstebo na Koplo wa Uhamiaji ambao
idadi yao ni 200, ambao walitakiwa kuripoti
tarehe 06 Agosti, 2014 lakini kwa sasa hawa
ndio wanaelekezwa wasubiri hadi hapo
watakapopewa maelekezo mengine.


Sgn
Isaac J. Nantanga
MSEMAJI WA WIZARA YA MAMBO YA NDANI
YA NCHI
29 JULAI, 2014

0 comments:

Post a Comment