Facebook

Friday 25 July 2014

Tetesi za usajili katika magazeti mbalimbali barani Ulaya.

Salim Kikeke's photo. Liverpool wapo tayari kumfuatilia tena Ryan Bertrand, 24, kutoka Chelsea, wakati Brendan Rodgers akisaka beki wa kushoto (Daily Mail)

kiungo wa Borussia Dortmund Marco Reus, 25, na beki wa Southampton Dejan Lovren, 25, ni miongoni mwa wachezaji Brendan Rodgers anawafuatilia (Daily Mirror)

Everton wanakaribia kumsajili Muhamed Besic, 21, kutoka Bosnia (Daily Mirror), 

Tottenham wanafikiria kumtaka beki Ron Vlaar, 29, wa Aston Villa, na wapo tayari kubadilishana na Lewis Holtby au Michael Dawson (Daily Mail), 

Chelsea wanamfuatilia kwa karibu beki Rafael Varane kutoka Real Madrid (Independent), 
 Salim Kikeke's photo.
Liverpool wana matumaini ya kuuteka mchakato wa uhamisho wa kiungo wa Juventus Arturo Vidal, 27, kwa kutoa dau la pauni milioni 42.5 walizotoa Manchester United (Metro),

Meneja wa Everton Roberto Martinez amethibitishwa kuwa anakaribia kumsajili David Henen, 18, kutoka Anderlecht (Talksport), 

AC Milan wanamfuatilia mshambuliaji wa Arsenal, Joel Campbell, 22, na tayari wamewasiliana na klabu hiyo ya London (Inside Futbol)

 Louis van Gaal anakabiliwa na mtihani mgumu baada ya Borussia Dortmund kumuonya kuwa asahau kumsajili Mats Hummels, 25 (Daily Express),

Manchester United 'wameruhusiwa' kumsajili winga wa Real Madrid Angel Di Maria, 26, baada ya timu hiyo kumsajili James Rodriguez kutoka Monaco (Caughtoffside) 

Hata hivyo taarifa nyingine zinasema Di Maria anataka kwenda PSG kwa mkopo kwanza kabla ya uhamisho wa kudumu msimu ujao (Daily Express), 

Boss wa Chelsea Jose Mourinho amewaambia makipa wake, Thiabaut Courtois, 22, na Petr Cech, 32, kuwa hawaendi popote, watake wasitake (Times),
 Salim Kikeke's photo.
Arsene Wenger yuko tayari kuacha kutafuta kiungo mwingine, na atamuamini Jack Wilshere, 22 (Daily Mirror),
 Salim Kikeke's photo.
 Boss wa QPR, Harry Redknapp anataka kumsajili mshambuliaji wa zamani wa Chelsea Samuel Eto'o (Daily Mirror)

Romelu Lukaku wa Chelsea, 21, anakaribia kuondoka Darajani baada ya kufanya mazoezi na klabu yake ya zamani Anderlecht (Sun).

0 comments:

Post a Comment