Facebook

Thursday 24 July 2014

Ahukumiwa kifungo cha miaka 77 kwa kuua Faru Afrika Kusini.

 Photo: JELA MIAKA 77 KWA KUUA FARU
Mtu aliyewinda na kuua faru watatu nchini Afrika Kusini amehukumiwa kwenda jela kwa miaka sabini na saba. Hii ni adhabu kuwa kuwahi kutolewa kwa kosa kama hilo. Mandla Chauke aliwapiga risasi watoto wa faru katika hifadhi ya wanyama ya Kruger mwaka 2011. Katika tukio hilo, mapigano ya risasi yalizuka kati ya majangili hao na walinzi wa hifadhi, ambapo mmoja wa washirika wa Chauke aliuawa, na yeye kukutwa na hatia ya mauaji yake. Afisa mmoja wa bodi ya hifadhi za taifa Afrika Kusini amefurahia hukumu hiyo akisema mahakama zimetambua athari za uwindaji haramu katika uchumi unaotegemea utalii. Pembe ya faru inaweza kuuzwa kwa dola laki moja na nusu katika masoko ya kimagenndo katika maeneo ya Asia. Watu wengi nchini China na Vietnam wanadhani pembe hizo zina tibu maradhi mbalimbali, ingawa hakuna ushahidi wa kisayansi kuhusu hilo.
Mtu aliyewinda na kuua faru watatu nchini Afrika Kusini amehukumiwa kwenda jela kwa miaka sabini na saba. Hii ni adhabu kuwa kuwahi kutolewa kwa kosa kama hilo. 
 
Mandla Chauke aliwapiga risasi watoto wa faru katika hifadhi ya wanyama ya Kruger mwaka 2011. Katika tukio hilo, mapigano ya risasi yalizuka kati ya majangili hao na walinzi wa hifadhi, ambapo mmoja wa washirika wa Chauke aliuawa, na yeye kukutwa na hatia ya mauaji yake. 
 
Afisa mmoja wa bodi ya hifadhi za taifa Afrika Kusini amefurahia hukumu hiyo akisema mahakama zimetambua athari za uwindaji haramu katika uchumi unaotegemea utalii. Pembe ya faru inaweza kuuzwa kwa dola laki moja na nusu katika masoko ya kimagenndo katika maeneo ya Asia. 
Watu wengi nchini China na Vietnam wanadhani pembe hizo zina tibu maradhi mbalimbali, ingawa hakuna ushahidi wa kisayansi kuhusu hilo.

0 comments:

Post a Comment