Facebook

Thursday 31 July 2014

Taarifa mbalimbali za Michezo kutoka ukurasa wa Wapendasoka facebook.


Kiungo wa Southampton Morgan Schneiderlin ameandika barua rasmiya kuomba kuondoka klabuni hapo baada ya uongozi wa klabu hiyo kutoa taarifa kwamba hawatouza mchezaji mwingine yeyote msimu huu.

Mpaka hivi sasa tayari Saints wameuza wachezaji wao kadhaa muhimu katika kikosi chao cha kwanza, hali ambayo inawashitua wengi ikiwemo nyota kadhaa waliosalia kuhusu mustakabali wa timu hiyo msimu ujao.

Aliyewahi kuwa kocha wa Southampton Mauricio Pochetino anatajwa kumshawishi kiungo huyo ajiunge na Tottenham Hotspurs ambayo anaifundisha hivi sasa. Iwapo Schneiderlin ataondoka, ataongezeka kwenye orodha ya wakali wa Southampton walioamua kusema kwaheri msimu huu ambao ni pamoja na Luke Shaw
aliyejiunga na Manchester United kwa dau la £27milioni,
Adam Lallana na Rickie Lambert waliotimkia Liverpool kwa
£25milioni na £4milioni, na Calum Chambers aliyejiunga na Arsenal kwa £16milioni.
Inasemekana pia Pochetino anataka kumsajili Jay Rodrigues kutoka Saints. Unaionaje Soton msimu ujao?

 
 Chelsea wamewakata maini Everton baada ya kupadisha bei ya mshambuliaji Romelu Lukaku kufikia £30 milioni.
Awali, Everton walitoa ofa ya £21 milioni kwa ajili ya Lukaku ambaye inasemekana Chelsea hawana mpango wa kumuuza.
Klabu ya Wolfsburg ya Ujerumani na Inter Milan ya Italia ni kati ya Klabu zinazomhitaji Lukaku kwa mkopo tofauti na Everton inayomhitaji kwa uhamisho wa moja kwa moja.

 Photo: Control Time. #Gambler - Hi Viz warriorfootball.com/boots/gambler
Klabu ya Napoli ya nchini Italia inafanya kila liwezekanalo kuhakikisha inamnasa kiungo asiyepata hewa nzuri katika klabu ya Manchester United Marouane Fellaini kwa mkopo.
Manchester United wapo tayari kumwachia Fellaini lakini wanataka kumuuza moja kwa moja na siyo kwa mkopo kama wanavotaka Napoli.


KOMBE LA EMIRATES MWAKA 2014 ARSENAL, MONACO,BENFICA NA VALENCIA UWANJANI.
Michuano ya kombe la Emirates inayoandaliwa na klabu ya Arsenal katika uwanja wa Emirates mwaka huu itafanyika Jumamosi na jumapili Wiki hii yani Tarehe 2 na tarehe 3 mwezi Agosti.

Wenyeji Arsenal watawaalika mabingwa wa Ureno Klabu ya Benfica, Kutoka Ufaransa ni Monaco na Spain itawakilishwa na Valencia.
Hii ni mara ya 7 michuano hiyo ikifanyika kama njia ya kuziandaa klabu husika hasa Arsenal kabla ya kuanza msimu mpya wa Ligi.

Mechi nne zitapigwa katika siku hizo mbili Jumamosi mechi ya kwanza itakua kati ya Monaco na Valencia halafu badae Arsenal watacheza na Benfica.
Jumapili mechi ya kwanza itakua kati ya Benfica na Valencia kabla ya Arsenal hawajamaliza kwa kuialika Monaco ya Ufaransa.

Timu itakayopata pointi nyingi ndiyo itakua Bingwa na utaratibu wa kugawa pointi ni timu itakayopata Ushindi itapata pointi 3, droo pointi 1 na kila goli litahesabiwa pointi moja.

RATIBA KAMILI
Jumamosi
14:00 Valencia vs Monaco
18:20 Arsenal vs Benfica

Jumapili
14:00 Benfica vs Valencia
18:20 Arsenal vs Monaco 

  El Apache





Baba mlezi wa mshambuliaji wa Juventus Carlos Tevez ameachiwa huru baada ya kutekwa wakati akiendesha gari akiwa umbali wa km 30 kutoka mji mkuu wa argentina,buenos aires!
Baba mlezi uyo alimlea carlos baada ya baba yake tevez kuuawa.
Carlos tevez baada ya tukio klabu yake imempa ruhusa kwenda argentina kutatua tatizo ilo.
Inasemekana watekaji wamepewa euro 30,000.
Matukio ya utekaji yamekuwa ya kawaida,kwani mwaka 2002,aliekuwa kiungo wa barcelona,juan roman riquelme ndugu yake alitekwa na ikamlazimu kutoa euro 95,000 ili ndugu yake aachiwe.
Mbona usikii rooney katekwa?
Kweli wale masikini wenzetu!
Umaskini nao mbaya sana,

 
Sijui liverpool wameona nini kwa uyu dogo!!?
Klabu ya liverpool imemsajili mshambuliaji kinda mwenye miaka 19 raia wa Ubelgiji,Divock Origi kwa ada ya euro 10,000,000 kutoka club ya ligue 1 lille.
Origi ambae ana asili ya kenya alikuwemo kwenye kikosi cha ubelgiji kilichofika hatua ya robo fainali kombe la dunia 2014 kule brazil.
Ubelgiji ilitolewa na argentina kwa kufungwa goli 1-0 kwa goli la gonzalo higuain.
Origi alianza kuichezea klabu ya genk kabla ya kusajiliwa na lille akiwa na umri wa miaka 15.
Pamoja na kusajiliwa divock oligi,klabu yake mpya imemuacha kule kule lille acheze kwa mkopo mpaka msimu wa 2015 ndiyo atajiunga na majogoo wa liverpool.
Liverpool inahaha kumtafuta mrithi wa luis suarez aliesajiliwa na klabu ya spain,fc barcelona kwa uhamisho wa euro 70,000,000 na kufanya awepo kwenye orodha ya wachezaji ghali duniani.
Record ya dunia bado inashikiliwa na Bale

 
Kiungo wa timu ya Taifa ya Uingereza Ross Barkley ameisaini mkataba mpya kuendelea kuitumikia timu yake ya Everton
Barkley mwenye miaka 20 alihusishwa kuihama club hiyo, ambapo vilabu vya Manchester United na City vilikuwa vinamnyemelea lakini hitimisho limefika mwisho.
Mchezaji huyo Amesaini Mkataba mpya wa miaka minne (4) kuendelea kukipiga Klabuni hapo hadi 2018.
Mkataba Utamfanya awe analipwa £65 000 kwa wiki. 


 Source:Wapendasoka-Kandanda (Facebook Page)

0 comments:

Post a Comment