Facebook

Monday 28 July 2014

Taarifa mbalimbali za Michezo kutoka ukurasa wa Wapendasoka.

 Wapenda SOKA - Kandanda
ATLETICO MADRID WAMSAJILI GRIEZMAN
..Mabingwa wa Spain Atletico Madrid wameendelea kuimarisha kikosi chao kwa kumsajili mshambuliaji mfaransa aliyekua akikipiga katika klabu ya Real Sociedad Antoinne Griezmann kwa ada ya uhamisho wa paundi milion 24.

Griezman anaelekea Madrid kuungana na Mario Mandzukic aliyesajili pia na klabu hiyo kutokea Bayern Munich mapema mwezi uliopita na wakali hao watatakiwa kuziba mapengo ya Diego Costa aliyetimkia Chelsea na David Villa aliyeenda Australia kumalizia soka lake.


Mmliki nα Rαis wα Αс Мilαn Silvio Berlusconi αmeripotiwα kutofurαhishwα nα kipigo wαlichopαtα dhidi yα Mαnchester city.

Rossoneri jana walifungwa na Man city mabao 5-1,ikiwa ni kipigo cha pili mfululizo kwenye Ziara yao Nchini Marekani baada ya kupoteza mechi ya kwanza Mbele ya Olympiacos.
Miezi 12 iliyopita Ac Milan ilfungwa goli 5 kwa 3 na Man City kwenye AUD CUP Nchini Ugeruman matokeo ambayo yanaendana na ya jana na Kumfanya Berlusconi kulichukulia suala hilo Kwa hisia Mbaya.  


LIVERPOOL WAACHANA NA REMY
Klabu ya Liverpool ambayo ilishakamilisha kila kitu ikiwemo ada ya uhamisho kutoka QPR wa mshambuliaji mfaransa Roic Remmy imeachana na mpango huo kwa sababu ambazo hazijawekwa wazi.
Taarifa kutoka kwa watu wa ndani ya Liverpool zinasema kuwa mshambuliaji huyu hakupasi vipimo vya afya, lakini watu wa karibu na mwanasoka huyo wanakanusha vikali taarifa hizo wakidai sababu ya kukwama kwa usajili huo ni mshambuliaji Fabio Borini ambae amekataa kujiunga na Sunderland na anataka kusalia Liverpool.


MATOKEO YA MECHI ZA JANA KATIKA SOKA

> INTERNATIONAL CHAMPIONS CUP

1. Man City 5-1 AC Milan
Wafungaji
Jovetic 12',58'
Sinclair 14'
Navas 23'
Iheanacho 26'
Muntari 42'

2. Liverpool 1-0 Olympiacos
Wafungaji
Raheem Stearling 4'

MECHI ZA KIRAFIKI

1. Essen 1-5 Borrusia Dortmund
Wafungaji
Aubameyang 8',10'
Subotic 22'
Mkhitaryan 25'
Immobile 30'
Soukou 39'

2. Ljubljana 1-2 Chelsea
Wafungaji
Kapun 40'
Diego Costa 56'
Zouma 64'
  

Dejan Lovren, beki mpya wa liverpool.
Photo: dejan lovren, beki mpya wa liverpool.

 
 Arsenal kumsajili beki kutoka southampton,chambers mwenye miaka 19.chambers ameshafanyiwa vipimo vya afya ijumaa iliyopita.
Kutoka academy ya southampton,chambers atakuwa mchezaji wa 3 kusajili na club ya arsenal baada ya walcot na chamberlain.
Inasemekana ada yake itakuwa ni £16mil.
Baadhi ya waandishi wa habari za michezo uingereza wanatabiri kijana uyo wenda akaenda kombe la dunia 2018 kule urusi.
Ujio wa chambers arsenal utafanya beki karl jenkinson apelekwe timu yoyote kwa mkopo ili akapate uzoefu wa kikosi cha kwanza.
Idadi wa wachezaji wa southampton inaongezeka kupungua baada ya Adam Lallana,Dejan Lovren,Lambert kwenda Liverpool na Luke shaw ameenda Man Utd.
Chambers anakuwa mcheza wa 4 kusajiliwa arsenal baada ya arsenal kuwasajili Sanchez,Debuchy na Ospina.


Bofya hapa ili uweze ku-like page ya facebook ya Wapendasoka na uweze kupata habari mbalimbali zinazohusiana na soka kwa muda na wakati muafaka :WAPENDA SOKA.

SOURCE:Wapendasoka/facebookpage

0 comments:

Post a Comment