Facebook

Wednesday 23 July 2014

Wachunguzi waanza kazi Ukraine,kuhsiana na ndege iliyoanguka.

Treni yenye mabaki ya waathiriwa wa mkasa wa ndege ya Malysia nchini Ukraine
Makubaliano ya kusitisha mapigano katika eneo ilipoanguka ndege ya Malaysia wiki iliyopita, yamefikiwa na pande zote kinzani , serikali ya Ukraine na wanamgambo wanaounga mkono Urusi.
Treni iliyobeba miili ya waliofariki katika mkasa huo wa ndege imewasili mjini Kharkhiv, mji unaodhibitiwa na serikali ya Ukraine, ikiwani ni siku 5 tangu kudunguliwa kwa ndege hiyo.
Kuhamishwa kwa masalia hayo ya ndege iliyoanguka MH17 inakuja baada ya shinikizo kali dhidi ya wapiganaji huku kukiwa na madai kuwa wao ndio walioindungua ndege hiyo.
Wanamgambo hao pia wamewakabidhi wachunguzi Vifaa vya rekodi mwenendo wa ndege hiyo- viitwavyo blackbox .
Mabaki ya ndege iliyoanguka
Uchunguzi wa kina unahitaji kufanywa kubaini nani hasa alihusika na undunguliwaji wa ndege hiyo.
Utawala wa Ukrain na nchi za magharibi zinadai wanamambo walisaidiwa na Urusi kuidungua ndege hiyo.
Wachunguzi wa kimataifa wameruhusiwa kuingia katika eneo la ajali baada ya baraza la usalama la UN kupitisha azimio.
Mwanachama mmoja wa kikundi cha wachunguzi, alisema kuwa wameweza kukata vipande vya mabaki ya ndege na kwamba kwa sasa wako katika eneo hilo.
Wanamgambo hao na Urusi wanakana vikali madai hayo.
Ndege hiyo ilianguka Alhamisi iliyopita na kuwaua watu 298.

0 comments:

Post a Comment