Facebook

Sunday 27 July 2014

Mgonjwa wa Ebola asakwa Sierra Leone


Mamlaka nchini Sierra Leone inataka usaidizi kutoka kwa raia wake ili kumsaka mgonjwa mmoja wa Ebola ambaye alichukuliwa kwa lazima na familia yake katika hospitali moja ya mji mkuu wa Freer Town.
Ni kisa cha kwanza cha ugonjwa huo katika mji huo uliojaa idadi kubwa ya watu, na kwamba radio za taifa hilo zimetoa habari zikiwaonya raia dhidi ya tishio la kumbukizwa iwapo watashikana na mwanamke huyo.
Kuna hofu kwamba ugonjwa wa Ebola huenda ukasambaa na kuingia nchini Nigeria.
Uchunguzi umethibitisha kwamba raia mmoja wa Liberia aliyefariki baada ya kutengwa katika hospitali moja ya Lagos alikuwa ameambukizwa ugonjwa huo.
Tangu kuzuka kwa ugonjwa huo mapema mwaka huu,zaidi raia 600 wamefariki kutokana na ugonjwa huo katika eneo la Afrika Magharibi.

0 comments:

Post a Comment