Facebook

Sunday, 27 July 2014

Gaza:Makubaliano ya saa 12 yaheshimiwa

Kiongozi wa Hamas na mwenzake wa Israel

Serikali ya Israel na wapiganaji wa Hamas wameanza kutekeleza makubaliano ya kusitisha vita kwa masaa 12 katika eneo la Gaza kutokana na maswala ya kibinidaamu.
Taarifa ya Israel imesema kuwa raia wa Palestina katika eneo la Gaza ambao walikuwa wameonywa kuondoka katika makaazi yao wasithubutu kurudi na kwamba Israel italipiza kisasi iwapo itashambuliwa.
Hatahivyo Israel imesema kuwa itaendeleza mashambulizi yake kuharibu mahanadaki yanayotumiwa na wapiganaji wa Hamas katika masaa hayo
Awali serikali ya Israel ilikataa makubaaliano ya kusitisha kwa mda mrefu yaliopendekezwa na waziri wa maswala ya kigeni nchini marekani John Kerry .
Bwana Kerry amesema ataendelea kushirikiana na katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban ki Moon ili kuafikiwa makubaliano ya kusitisha vita ya siku saba.
Bwana Ban amesema kuwa vita vinavyoendelea vinaonyesha wazi kwamba hakutakuwa na suluhu ya kijeshi na kwamba uzuiaji wa Gaza ni sharti usitshwe.
Zaidi ya raia mia nane wa palestina wameuawa pamoja na wa Israel zaidi 30.

Related Posts:

  • Mwanaume apata dalili za ujauzito Uingereza.Harry Ashby ni mwanaume wa kwanza nchini Birmingham kupata ruhusa ya kupumzika nyumbani baada ya kusumbuliwa na homa mithili ya mwanamke mja mzito. Amekuwa akipatwa na homa za vipindi hasa nyakati za asubuhi baada ya mchumba … Read More
  • "Mungu wa Kihindi" awekwa kwenye vitambulisho India.Maafisa wa utawala nchini India, wanachunguza ambavyo kitambulisho cha elektroniki kimetengezwa kikiwa na picha ya Hanuman mungu wa kihindi na kutumwa kwa njia ya posta. Kitambulisho hicho kina picha ya mtu anayejulikana kama… Read More
  • Boko Haram wauteka mji mkubwa wenye,watu wengi Nigeria.Wapiganaji wa kiisilamu wa Boko Haram wameuzingira mji wa Maiduguri , mji rasmi wa jimbo la Borno Kaskazini Mashariki ya Nigeria. Wazee wa vijiji wametahadharisha kuwa jeshi linahitaji kuweka ulinzi thabiditi katika mji huo a… Read More
  • Mchakato wa katiba kusitishwaKumekuwa na maoni tofauti kufuatia hatua ya kusitisha mchakato wa kura ya maoni ya Katiba Mpya nchini Tanzania. Katika kikao cha Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete na Viongozi wa vyama vya siasa nchini humo wamekubaliana kuwa ku… Read More
  • Mahakama yazuia unywaji Pombe India. Mahakama ya rufaa nchini India imezuia mpango wa jimbo la Kerala Kusini mwa nchi hiyo kupiga marufuku pombe. Mamia ya wamiliki wa baa walikuwa wamepinga marufuku hiyo ambayo ingeanza kutekelezwa Ijumaa hii kwa kusema kuwa … Read More

0 comments:

Post a Comment