Facebook

Thursday 31 July 2014

Yaya Toure "Nataka kubaki Etihad"



Yaya Toure anataka kusalia Etihad kwa miaka zaidi.
Kiungo cha kati wa Ivory Coast na Manchester City ya Uingereza Yaya Toure amesema kuwa angependa kusalia Etihad milele.
Awali ripoti zilikuwa zimeashiria kutoridhishwa kwake na jinsi anavyothaminiwa na wamiliki wa klabu hiyo bingwawa ligi kuu ya Uingereza.
Wakala wake Dimitry Seluk,alikuwa amenukuliwa akidai kuwa Toure alikuwa anahisi kutelekezwa na wenye klabu.
Lakini sasa Toure anasema kuwa swala wakati huo halikuwa uhamisho bali ilikuwa ni utatuzi swala ibuka.
Seluk alikuwa amesema kuwa wamiliki wa klabu hiyo walipuuza Toure siku ya kuadhimisha kuzaliwa kwake mwezi mei timu hiyo ilipokuwa ziarani katika Milki za Kiarabu .
Man City ilikuwa UAE kusherehekea ushindi wa ligi kuu ya Uingereza.
Wakati huo Toure alidhaniwa kutilia pondo matamshi ya wakala wake katika mtandao wa kijamii wa Twitter alipodai kuwa hakujuwa ataichezea klabu ipi msimu huu.


Seluk alisema Yaya angefurahia kukaa Etihad milele.
Sasa Toure mwenyewe amepuzilia mbali dhana kuwa alikuwa anapanga kuondoka Etihad akisema kuwa sasa anataka kusalia huko kadri anavyoweza.
Toure, ambaye alitia sahihi kandarasi ya miaka minne mwaka uliopita anapendekeza kusajiliwa kwa wachezaji wengine wapya ilikuimarisha klabu hiyo.
''ikiwa tunataka kuwa klabu yenye sifa lazima nasi tushinde mataji yote''

0 comments:

Post a Comment