Facebook

Thursday 24 July 2014

Arsenal yamnyatia Matija Nastasic wa Man City kuimarisha ukuta wao.

 Photo: Manchester City imepokea maombi ya vilabu vya Inter Milan na Roma kwa ajili ya Matija Nastasic ambaye wanataka kumuuza kwa lengo la kumsajili  Eliaquim Mangala akitokea katika klabu ya Porto.
Hata hivyo inaonekana vilabu hivyo huenda vikapigwa kumbo na Arsenal ambayo inataka kufanya malipo kwa haraka.
Ingawa Arsene Wenger ameshaweka wazi kwamba hategemei kununua mlinzi wa kati mzimu huu, lengo lake hilo linaweza kubadilika iwapo nahodha Thomas Vermaelen ataondoka na kujiunga na Manchester United.
Mlinzi huyo wa kimataifa wa Serbia alikaribia kuiunga na Arsenal alipokuwa akiitumikia Fiorentina, kabla ya City kumdaka mwaka 2012 na kuendeleza ubora wake kama mlinzi bora Ulaya. 
Kwa sasa City hawamuhitaji na inaonekana kwamba mchezaji mwenyewe na Arsenal wako tayari kurudisha matamanio ya kuungana.

Veramaelen aondoke aje Nastasic?
Manchester City imepokea maombi ya vilabu vya Inter Milan na Roma kwa ajili ya Matija Nastasic ambaye wanataka kumuuza kwa lengo la kumsajili Eliaquim Mangala akitokea katika klabu ya Porto.
Hata hivyo inaonekana vilabu hivyo huenda vikapigwa kumbo na Arsenal ambayo inataka kufanya malipo kwa haraka.
Ingawa Arsene Wenger ameshaweka wazi kwamba hategemei kununua mlinzi wa kati mzimu huu, lengo lake hilo linaweza kubadilika iwapo nahodha Thomas Vermaelen ataondoka na kujiunga na Manchester United.
Mlinzi huyo wa kimataifa wa Serbia alikaribia kuiunga na Arsenal alipokuwa akiitumikia Fiorentina, kabla ya City kumdaka mwaka 2012 na kuendeleza ubora wake kama mlinzi bora Ulaya.
Kwa sasa City hawamuhitaji na inaonekana kwamba mchezaji mwenyewe na Arsenal wako tayari kurudisha matamanio ya kuungana.

0 comments:

Post a Comment