Facebook

Saturday, 26 July 2014

Wanariadha wa Kenya walalamika Scotland.


Wanariadha wa Kenya wakiwa mjini Glascow
Kikosi cha Kenya katika mashindao ya Jumuiya ya madola, yanayoendelea mjini Glascow, kinakabiliwa na wakati mgumu, kutoka na matatizo kadhaa.
Sasa imebainika kuwa baadhi ya wanariadha wa Kenya hawana vifaa vya michezo.
Naibu kiongozi wa ujumbe wa Kenya Tecla Lorupe amesema kuwa wao walifahamishwa siku ya Alhamisi kuwa baada ya wanariadha hawajapokea vifaa na sare zao za michezo.
Lorupe ambaye, ni bingwa wa zamani wa dunia katika mbio za masafa marefu za Marathon, amesema wao wameshangazwa sana na tukio hilo.
Wanariadha wa Kenya katika mashindano ya Jumuiya ya Madola mjini New Delhi
Amesema kumekuwa na matatizo ya kuwasilisha vifaa hivyo vya wanamichezo wa Kenya, kutoka kwa kampuni inayotengeneza mavazi hayo.
Aidha amesema nusura mabondi wa Kenya wakose kushiriki katika mashindano ya mwaka huu, kutokana na ukosefu wa vifaa vyao.
Lorupe amesema walipata bahati wakati, kamishna wa michezo nchini Kenya Gordon Oluoch alipolazimika kutumia fedha fedha zake kununua vifaa hivyo ambavyo vilitumika na mabondia siku ya Ijumaa.
Siku ya Alhamisi, muogeleaji wa Kenya Jason Dunford aliondolewa katika shindano ya mita hamsini butterfly, kutokana na kile alichokitaja kama kutopata vifaa kwa wakati unaofaa.
Mbali na wanariadha kukosa vifaa na mavazi yao, wasimamizi wa michezo mbali mbali nao wanalalamika kuwa hawajapata marupurupu yao.
Hali hii imelleta wasi wasi katika kambi ya kenya huku baadhi ya wanariadha wakiondolewa mapema katika mashindano ya mwaka huu.
Tecla Lorupe
Baadhi yao wanasema, hali duni katika kambi ya maandalizi na hapa mjini Scotland huenda ikaadhiri matokeo ya timu ya Kenya.

Related Posts:

  • Yanga kupinga maamuzi ya TFF juu ya Okwi.Uongozi wa klabu ya Yanga umesema utapinga maamuzi ya kamati ya Sheria na Hadhi ya Wachezaji kuhusiana na maamuzi yake ya kumtangaza mchezaji wake, Emmanuel Okwi kuwa huru. Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria ya Yanga, Sam Mapande… Read More
  • Maicon aondolewa timu ya taifa ya Brazil kwa kashfa ya "Ushoga" Brazil ilicheza mechi ya kirafiki na Colombia kule Miami Florida, hapo jumamosi, ikaibuka na ushindi wa 1-0, kwa goli lililofungwa na mshambuliaji wa Neymar. Hivi sasa Brazil inajiandaa kukipiga na Ecuador hapo Jumatano, Se… Read More
  • FAIDA YA MAN UTD 'KUTETEREKA'Manchester United imetangaza kuporomoka kwa faida ya kila mwaka wa fedha katika mwaka ambao David Moyes alikuwa meneja. Klabu hiyo ya Ligi Kuu ya England imesema kipato halisi kimeporomoka kwa asilimia 84 na kufikia takriban … Read More
  • Danny Welbeck aing'arisha Uingereza.Danny Welbeck straika mpya wa Arsenal alifunga mara mbili kuisaidia England kuifunga Switzerland kwa bao 2-0 katika mchezo wa kufuzu michuano ya Euro 2016. Mchezaji huyo wa zamani wa Manchester United aliziona vyavu dakika ya… Read More
  • iPhone 6 Plus yatengenezwa kwa ajili ya Mashabiki wa Manchester United.Mashabiki ulimwenguni wamesema simu mpya aina ya iPhone 6 Plus imetolewa maalum kwa ajili ya mashabiki wa Manchester United ambayo kwenye simu ya kawaida haionekani kwa urahisi kwenye msimamo wa ligi kuu ya England lakini kup… Read More

0 comments:

Post a Comment