Facebook

Friday 25 July 2014

Aenda kutahiriwa,madaktari wakati "nanihii" yote

Salim Kikeke's photo.
Mtu mmoja mjini Alabama nchini Marekani amefungua kesi ya madai baada ya kudai kuwa alikwenda kutahiriwa lakini madaktari wakaondoa uume wake wote.
Tovuti ya Metro imesema Johnny Lee Banks Jnr anadai kuwa alikwenda kufanya 'suna' katika hospitali ya Princeton Baptist Medical Center na uume wake kukatwa kimakosa na madaktari.
Kesi hiyo iliyofunguliwa na Bwana Banks pamoja na mkewe Zelda, inasema bwana huyo hakupewa maelezo yoyote ya kwanini 'mashine' yake iliondolewa na wala hakuonywa kuwa shughuli ya kutahiri ina hatari na uwezekano wa kukatwa kabisa uume.
"Mshtaki alipozinduka kutoka kwenye dawa ya usingizi baada ya upasuaji, alikuta uume umekatwa," yamesema maelezo ya mashtaka.

Salim Kikeke's photo. "Mdai hakutoa idhini yoyote ya kukata kabisa au nusu ya uume wake,' imesema karatasi ya mashtaka.
Bwana huyo ameitaja hospitali, pamoja na madaktari wawili kuwa ndio washtakiwa katika kesi hiyo, akisema walikuwa wazembe na walishindwa kutafuta msaada walipopatwa na tatizo wakati wa upasuaji.

CHANZO: Metro

0 comments:

Post a Comment