Facebook

Thursday 24 July 2014

Tetesi za usajili katika magazeti mbalimbali barani Ulaya.

 Salim Kikeke's photo.

Meneja mpya wa Manchester United Louis van Gaal ameambiwa kuwa anaweza kutumia kiasi chochote cha fedha kusajili wachezaji wapya Old Trafford na hata kuvunja rekodi za uhamisho (Guardian),

 Salim Kikeke's photo.
 Man U Pia wametajiwa kuwa wanaweza kuendelea kumsaka Angel Di Maria, 26, kufuatia Real Madrid kumsajili kiungo mshambuliaji James Rodriguez, 23, kutoka Monaco (Independent),

Arsenal wamekubali ada ya uhamisho ya pauni milioni 3 kumsajili kipa wa David Ospina, 25 kutoka Nice ya Ufaransa (Guardian),

Boss wa Liverpool Brendan Rodgers anataka kumsajili beki wa kulia Javier Manquillo, 20, kutoka Atletico Madrid kwa mkopo. Mchezaji huyo anawindwa pia na Arsenal (Sun), 

Atletico Madrid wanawanyatia wachezaji wawili wa Arsenal, Santi Cazorla na Nancho Monreal (Daily Telegraph), 

Arsenal wamerejea kumyatia kiungo wa Sporting Lisbon William Carvalho, 22, baada ya mazungumzo ya kumchukua Sami Khedira wa Real Madrid, 27, kusuasua (Daily Star),

Tottenham na Arsenal wanaonesha nia ya kumsajili kiungo mshabuliaji Douglas Costa, 23, kutoka Shakhtar Donetsk. Mchezaji huyo kutoka Brazil amekataa kurejea Ukraine kutokana na matatizo ya kisiasa katika nchi hiyo (Independent),

Mshambuliaji Divock Origi, 19, amesafiri kwenda Marekani kukamilisha usajili wake wa Liverpool, lakini atabakia Lille kwa msimu ujao (Daily Express),

Uwezekano wa Didier Drogba, 36, kurejea Chelsea huenda kukasababisha Romelu Lukaku kuondoka Darajani, na huenda akaenda Everton (Daily Telegraph), 

Everton wameripotiwa kukaribia kumsajili David Henen, 18, kutoka Anderlecht (Liverpool Echo), 

Inter Milan wako makini kumsajili mshambuliaji wa Manchester United Javier Hernandez, baada ya kuambiwa na Manchester City kuwa Stevan Jovetic, 24, hauzwi (Sun),

Hull City wanazungumza na beki wa kimataifa kutoka Cameroon Jean-Armel Kana-Biyik, 25 kutaka kumsajili kutoka Rennes ya Ufaransa (Sky Sports), 

 Lionel Messi, 27, 'alitishia' kujiunga na Arsenal msimu uliopita, wakati akizungumzia mkataba wake mpya na Barcelona (Daily Mail),

Luis Suarez, 27, ameukimbia mji wa Barcelona, kuwaepuka waandishi wa habari wanaomfuatilia kwa karibu (Daily Star), 

Manchester United wanajiandaa kutoa pauni milioni 39 kumchukua Arturo Vidal, 27, kutoka Juventus (Tuttosport),

 klabu ya Eintracht Frankfurt ya Ujerumani imefuta mazungumzo na mshambuliaji wa zamani wa Arsenal Nicklas Bendtner, 26, kwa sababu mchezaji huyo anataka mshahara mkubwa (Le Figaro),

Meneja wa Borussia Dortmund Jurgen Klopp ametupilia mbali tetesi kuwa beki Mats Hummels, 25, anakwenda Manchester United, na kiungo Marco Reus, 25 anakwenda Bayern Munich (Bild), 
 Salim Kikeke's photo.
Atletico Madrid wanashindwa kutoa pauni milioni 13 wanazotaka Chelsea kumsajili Fernando Torres, 30, licha ya kuwa meneja Diego Simione kutaka sana kumchukua (AS). 

0 comments:

Post a Comment