Facebook

Thursday 24 July 2014

Aliyefunga alazimishwa kula,azua mzozo mkubwa India

Waislamu hufunga kula na kunywa mpaka jua linapozama
Mzozo umeibuka kwenye Bunge la India baada ya kuwepo Ripoti kuwa baadhi ya Wabunge wa dini ya Hindu walijaribu kumshurutisha mtu mmoja aliyekuwa kwenye mfungo wa Ramadhan kula chakula.
Wabunge hao kutoka mrengo wa kulia wa Chama cha Shiv Sena wameripotiwa kuwa walikuwa na hasira kwa kuwa hawakupatiwa chakula walichokichagua katika mgahawa wa Serikali.
Waislamu duniani kote wanafunga kula na kunywa kabla ya jua kuzama katika kipindi cha mfungo.
Vyama vya upinzani vikiongozwa na chama cha Congress wamekemea kitendo hicho wakisema ni ukiukwaji wa imani ya dini,na kutaka chama cha Shiv Sena kuomba radhi.

Kwa mujibu wa Ripoti, tukio hilo lilitokea jumanne mjini Delhi baada ya wabunge kadhaa kutoka chama cha Shiv Sena cha jimbo la Maharashtra kuchukizwa na hali ya kutokuwepo kwa chakula walichokitaka na kutumia nguvu kusokomeza kipande cha mkate mdomoni mwa mfanyakazi wa mgahawa aliyekuwa katika mfungo.

Gazeti la Indian Express limesema baada ya tukio hilo, kazi katika mgahawa huo zilisimama, huku msimamizi wa mgahawa akilalamika kuwa mfanyakazi huyo amesikitishwa sana na kitendo hicho.
Chama cha Shiv Sena kimekana kuhusika kwenye tukio hilo kikidai kuwa njama za kisiasa.

0 comments:

Post a Comment