Facebook

Wednesday 30 July 2014

Tetesi za usajili katika magazeti mbalimbali barani Ulaya.


Salim Kikeke's photo.
Kiungo wa Manchester United Marouane Fellaini huenda akaondoka kwenda Napoli baada ya kufanya mazungumzo na mkuu wa klabu hiyo Riccardo Bigon (Daily Express),
 Salim Kikeke's photo.
United pia huenda wakamruhusu Shinji Kagawa, 25 kuondoka huku Borussia Dortmund wakiwa tayari kumchukua tena (Independent), 
Chelsea watalazimika kumuuza kipa Petr Cech, 32, kwenda PSG iwapo watashindwa kumuuza Fernando Torres, 30, au John Obi Mikel, 27 (Daily Telegraph),
 Salim Kikeke's photo.
Meneja wa Southampton Ronald Koeman ana matumaini ya kumsajili kiungo Serge Gnabri, 19 na Carl Jenkinson, 22 kutoka Arsenal (Daily Star),
Hata hivyo Southampton wanakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa West Ham wanaokaribia kumchukua Jenkinson kwa mkopo (Daily Mirror), 
Beki wa kulia wa Sporting Lisbon Miguel Lopez, 27 anajiandaa kujiunga na Tottenham kwa mkopo, huku akitazamia uhamisho wa kudumu baadaye (Daily Mail), 
Meneja wa Liverpool Brendan Rodgers amethibitisha kuwa hawatopanda dau tena kumchukua Loic Remy (Daily Mirror), 
Lakini Newcastle United huenda wakajaribu kumchukua tena Remy kwa mkopo (Goal.com)
Meneja wa Aston Villa Paul Lambert anataka kumsajili Victor Moses, 23, kwa mkopo na pia kumchukua Ki Sung-yeung, 25 kutoka Swansea wiki hii (Daily Telegraph), 
 Salim Kikeke's photo.
Wakala wa Samuel Eto'o amewaambia West Ham kuwa mchezaji huyo yuko huru kujiunga nao, kuziba pengo la Andy Carroll aliyeumua, lakini Eto'o anataka mshahara wa pauni 100,000 kwa wiki (Daily Mail), 
Mkurugenzi mkuu wa Juventus Beppe Marotta amesema klabu yake itajitahidi kutomwachilia Arturo Vidal, na kutupilia mbali taarifa kuwa mchezaji huyo anakwenda Chelsea (Tottosport), 
Southampton wanafikiria kumchukua beki wa kati wa Sporting Lisbon Marcos Rojo, 24, kufutia kuondoka kwa wachezaji wengi Saints (Le Figaro), 
Atletico Mineiro amethibitisha kuondoka kwa kiungo wa zamani wa Barcelona Ronaldinho, 34 (L'Equipe), 
Mshambuliaji wa Ubelgiji Divock Origi, 19, amesaini mkataba wa miaka mitano na Liverpool (Bild),
PSG wameruhusu mshambuliaji wao Ezequiel Lavezzi, 29, kwenda Atletico Madrid. Mchezaji huyo anasakwa pia na Liverpool (AS.com)
Lazio ya Italia imetangaza kuwa inamchukua beki wa Feyenoord Stefan de Vrij, 22 (L'Equipe)

0 comments:

Post a Comment