Facebook

Saturday 26 July 2014

Mama anayeugua Ebola atoroshwa

Mwanamke aliyeambukizwa Ebola atoroshwa Hospitalini huko Freetown
Hali ya Tahadhari imetangazwa mjini Freetown Sierra Leone baada ya mwanamke mmoja aliyeambukizwa Ebola kutoroshwa kutoka Hospitalini na jamaa zake kwa hofu kuwa angekufia huko.
Maafisa wa Usalama wa Umma na wale wa Afya wanaendelea kumtafuta wakitumia vyombo vya habari na hata redio kutangaza kuwa kuwepo kwake nje ya Hospitali na hatari kwa afya ya umma.
Mama huyo ndiye aliyekuwa wa kwanza kudhibitishwa kuugua Ebola mjini Freetown.
Mama anayeugua Ebola atoroshwa hospitalini Freetown
Wakati huohuo Mwanamume mmoja aliyekuwa anafanyiwa uchunguzi nchini Nigeria kujua iwapo anaugua ugonjwa wa Ebola ameaga dunia.
Mwanume huyo ambaye ni raia wa Liberia, aliwasili Jumapili Lagos, kupitia Togo na mara akaanza kuugua na ugonjwa unaofananishwa na Ebola.
Mgonjwa huyo alikuwa ametengwa ilikufanyiwa uchunguzi kwani hakujakuwa na mgonjwa yeyote wa Ebola nchini Nigeria licha ya Ugonjwa huo kuenea kote katika mataifa ya magharibi mwa Afrika.
Iwapo itadhibitishwa kuwa alikuwa anaugua Ebola basi yeye ndiye atakayekuwa mgonjwa wa kwanza wa Ebola nchini humo.
Zaidi ya watu 600 wamefariki kutokana na Ebola magharibi mwa Afrika tangu mwezi February.
.Mlipuko wa ugonjwa huo hatari ulianza huko Guinea na kuenea hadi Liberia na Sierra Leone.
Virusi vya ugonjwa huo husababisha uvujaji mwingi wa damu na katika zaidi ya nusu ya visa vilivyoripotiwa, waathiriwa wamefariki. Hakuna chanjo dhidi Ebola .

0 comments:

Post a Comment