Facebook

Thursday 24 July 2014

Manchester United yaanza kuwa tishio ndani ya muda mfupi.

Photo: Venue: Rose Bowl......7-0?
Formation 3-5-2

Kuna kitu nakiona kinakuja pale Old Trafford ujio huu wa Van Gaal ni tofauti kabisa na anguko lile la David Moyes.

Kipindi kama hiki Moyes alianza kibarua kwa kichapo cha bao 1-0 toka kwa kombaini ya Hongkong,muda mfupi uliopita Van Gaal kashusha kichapo cha paka mwizi kwa Galaxy katika dimba la Rose Bowl.

Amewatumia Jones,Smalling na Evans kama walinzi huku Shaw na Valencia wakicheza kama wing-backs kikosi kimeonekana kubalance vizuri mno huku Ander Herrera akianza kuthibitisha thamani yake nadhani mpira umetabasamu mara nyingi zaidi ulipofika miguuni kwake.

Waswahili wanasema siku nzuri huonekana asubuhi,naiona Manchester haswa tena ya kiajax na kibayern siyo ile ya kieverton.

Kweli Van Gaal uchichimame wala uchikae......
Kuna kitu nakiona kinakuja pale Old Trafford ujio huu wa Van Gaal ni tofauti kabisa na anguko lile la David Moyes.

Kipindi kama hiki Moyes alianza kibarua kwa kichapo cha bao 1-0 toka kwa kombaini ya Hongkong,muda mfupi uliopita Van Gaal kashusha kichapo cha paka mwizi kwa Galaxy katika dimba la Rose Bowl.

Photo: Rooney akifunga goli la pili kwa njia ya penati.

via-Ayo's 
Amewatumia Jones,Smalling na Evans kama walinzi huku Shaw na Valencia wakicheza kama wing-backs kikosi kimeonekana kubalance vizuri mno huku Ander Herrera akianza kuthibitisha thamani yake nadhani mpira umetabasamu mara nyingi zaidi ulipofika miguuni kwake.

Photo 
Ander Herrera akikabidhiwa tuzo ya mchezaji bora wa mechi
 
Mechi ya kwanza kwa kocha Mpya wa Man United Luis Van Gaal imemalizika kwa ushindi mkubwa wa Bao 7-0.

Akichezesha vikosi viwili yani kila kipindi kikosi chake isipokua kwa Ander Herrera na Darren Fletcher ambao wao walimaliza dakika zote 90,United ilipata goli 3 mpaka mapumziko magoli mawili ya Wayne Rooney dakika ya 41 na 45 lakini kabla ya hapo Danny Welbeck aliingia katika historia kwa kufunga goli la kwanza katika utawala wa kocha Van Gaal dakika ya 13.

Kipindi cha Pili United iliingiza chipukizi walioungana na wakongwe kuimaliza LA Galaxy wakifanikiwa kupata goli la 4 na la 5 yakifungwa na Reece Wilson ambaye aliingia kuchukua nafasi ya Luke Shaw baada ya kazi nzuri ya Ashley Young.

Photo: Louis van Gaal was delighted with United's 7-0 win vs LA Galaxy. "It's fantastic how they performed. [The score] was a surprise but they were beautiful goals!" 
Ander Herrera ambaye amecheza mechi yake ya kwanza leo alionekana ndo bora kabisa katika mchezo huo kwa kumtengenezea Ashley Young ambaye bila ajizi alifunga magoli mawili dakika ya 88 na 90.

Photo: FT: LA Galaxy 0 United 7. Louis van Gaal gets his Reds reign off to the perfect start as goals from Danny Welbeck, Wayne Rooney (2), Reece James (2) and Ashley Young (2) seal a crushing win in the opening #mutour game in Pasadena.  Head to our Twitter page for post-match reaction: http://bit.ly/1kuZJw2 
 Kabla ya mechi hiyo Manchester City nao walifanikiwa kuifunga Sporting Kansa City bao 4-1.

Waswahili wanasema siku nzuri huonekana asubuhi,naiona Manchester United haswa tena ya ki-Ajax Amsterdam na ki-Bayern Munich siyo ile ya ki-Everton.

Kweli Van Gaal uchichimame wala uchikae......
 
  Imeandaliwa na.........
                                      Katemi P. Methsela

0 comments:

Post a Comment