Facebook

Friday 5 December 2014

ICC yaitupilia mbali kesi ya Uhuru Kenyatta.

Mahakama ya kimataifa ya ICC imetupilia
mbali kesi ya jinai inayomkabili Rais wa
Kenya Uhuru Kenyatta.
Mwendesha mkuu wa mashitaka Fatou
Bensouda ameondoa kesi dhidi ya Kenyatta
ambaye alidaiwa kutenda uhalifu dhidi ya
binadamu wakati wa ghasia za baada ya
uchaguzi mwaka 2007/2008.

Mahakama ilikuwa imempa Bensouda wiki moja
kuamua ikiwa ataendelea na kesi dhidi ya
Kenyatta au la inagwa alisema muda huo
haukutosha kwake yeye kuandaa ushahidi zaidi
dhidi ya Kenyatta.
Kenyatta alishtakiwa kama mshukiwa mkuu wa
ghasia za baada ya uchaguzi wa 2007/2008
akituhimiwa pamoja na William Ruto ambaye ni
naibu Rais kwa kutenda uhalifu dhidi ya
binadamu.

Zaidi ya watu elfu moja waliuawa wakati wa
ghasia hizo. Uhuru alikuwa mtu maarufu zaidi
kufikishwa mahakamani na pia mshukiwa mkuu
kwani alifikishw amahakamani akiwa Rais aliye
mamlakani.
Hili ni pigo kubwa kwa upande wa mashitaka,
wengi wlaioana keshi dhidi ya Kenyatta kama
mtihani mkubwa katika historia ya mahakama
hio.

Upande wa mashitaka ulitaka mahakama
kuupatia muda zaidi ili upate ushahidi
zaidi,dhidi ya Kenyatta kama vile taarifa za
akaunti yake ya benki.
Upande wa utetezi uliteta kuwa ikiwa hakuna
ushahidi wa kutosha kesi hio inapaswa
kutupiliwa mbali.

0 comments:

Post a Comment