Facebook

Sunday 7 December 2014

NI MUDA MUAFAKA WA LUIS VAN GAL KUUMPA NAFASI FALCAO KWENYE KIKOSI CHA KWANZA

Nadhani falcao anahitaji dakika 90 akiwa na jezi ya United.
Van persie anapewa muda mwingi wa kucheza,amekuwa katika kikosi cha kwanza kwa asilimia 90  katika michezo 14 ya united msimu huu.kwanini asifunge ?

Anacheza mbele ya Di maria,Ander Harrera ,Muan Mata na Rooney, anapata nafasi ngapi ..!? Anafunga ngapi? Kwa dakika alizocheza na nafasi alizopata, Van Persie hakustahili kufunga mabao manne tu!

Huu ni muda muafaka sasa wa Luis Van Gal kuelekeza upepo kwa Falcao timu inahitaji mabao mengi kwa sasa na kwa jinsi inavyoonekena miguu ya Van Persie imepoteza jicho la goli kwa ufupi jamaa kaisha au anaelekea kuisha kabisa.

Manchester United inahitaji mabao kwa aina ya washambuliaji wulionao  Rooney,Van Persie na FALCAO kwanini ikose magoli  zaidi ya 70 kwa msimu huu hapa kuna tatizo na tatizo kubwa ni Van Persie

Tayari Falcao ameshapewa miezi minne ya mwisho kudhihirisha ubora wake.

Lakini ni kichekesho kwa Falcao kuumpa muda huu,hali yakuwa anatumia muda mwingi kukaa kwenye benchi la Luis Van Gaal

Kwa van persie tumeshaona makali na udhaifu wake,muda huu ambao  Falcao ameshapona,ni wakati mzuri  kwa Luis Van Gaal kutupa karata kwa Radamel Falcao EL TIGRE.

Kama ningekua na uwezo ningemshauri van Gal amuanzishe FALCAO mechi ya kesho dhidi ya Southampton.

Nawasilisha.

0 comments:

Post a Comment