Facebook

Friday 5 December 2014

Waishi na maiti wakiamini itafufuka kwa maombi Canada

Familia moja nchini Canada iliishi na maiti
katika chumba cha juu cha nyumba yao
kwa miezi sita kwa kuwa waliamini
marehemu atafufuka iwapo wataendelea
kumuomba mungu,lakini mwili huo
ukapatikana baada ya familia hiyo
kushindwa kulipa mkopo waliochukua
kununua nyumba hiyo.

Kaling Wald mwenye umri wa miaka 50
alipatikana na makosa ya kushindwa kuwaarifu
maafisa wa polisi kwamba mumewe
alifariki ,kosa ambalo na akahukumiwa
kuwekwa katika muda wa majaribio na
ushauri,wakili wake alikiambia chombo cha
habari cha Reuter siku ya Jumanne.
Peter Wald mwenye umri wa miaka 52 alifariki
mnamo mwezi machi mwaka 2013 kwa kile
mamlaka inasema ni sababu za kawaida
kufuatia maambukizi ya mguu wake
yanayodaiwa kusababishwa na ugonjwa wa
sukari.
Mkewe Kaling Wald alimwacha kitandani na
kufunga chumba hicho katika nyumba yao ya
Hamilton ,Ontario ili kuzuia harufu kali
iliokuwa ikitoka chumbani humo kuwafikia
watu waliokuwa wakiishi nyumbani humo.

Kama vile Yesu alivyomfufua Lazaro baada ya
siku ya nne ,pia yeye aliamini kwamba Mungu
atamfufua mumewe wakili wa mwanamke huyo
alisema.

0 comments:

Post a Comment