Facebook

Tuesday, 9 December 2014

Huyu ndiye mwanamke anayeishi kwa kuuza "maziwa ya mama"


 
Rebecca Hudson, kutoka mjini Manchester,Uingereza amepata zaidi ya pauni 3,000 kwa kuuza maziwa ya mama.
Mama huyo mwenye umri wa miaka 26, anasema kuwa wakati mwanawe alipozaliwa mapema mno , wiki kumi kabla ya siku iliyotarajiwa, matiti yake yakawa hayawezi kutoa maziwa.
Lakini baadaye alianza kupata maziwa mengi sana kupita kiasi.

Na kwa sababu mtoto wake alizaliwa kabla ya siku yake, alihitaji tu kutoa maziwa kidogo kama chakula cha mtoto wake aliyekua katika mashine hospitalini.
Alisema ''sikutaka kuyamwaga maziwa yaliyosalaa, kwa sababu ni kazi ngumu sana kwa mama kutoa maziwa kwenye Matiti yake.''
"kwa hivyo nilitafakari ili niweze kupata pesa za ziada, sioni ubaya wowote ikiwa nitayauza maziwa yangu. ''
 

Kwa hivyo Rebecca alikwenda kwenye mtandao wa Internet, na kugundua kuwa nchini Marekani kuna wanawake ambao tayari wanauza maziwa hayo. Hapo ndipo aliamua kuanza kuuza maziwa yake kwenye mtandao.

Ana wateja ambao yeye huwauzia maziwa yake kwa pauni 12.50 kwa kila chupa.
Wateja wake wengi huwa ni wanyanyuaji uzani ambao hutumia maziwa hayo yanayosemekana kuwa na madini muhimu sana kwa mwili, pamoja na wapishi ambao hutumia maziwa hayo kwa upishi. Kadhalika watu hununua maziwa hayo wakiamini kuwa inawapa nguvu za kimwili na kuwaezesha kingono.

Rebecca Hudson alisema kuwa kwake yeye kile ambacho wateja wake wanatumia kufanyia maziwa ni shauri yao, ''sitabagua na kuwauzia watu fulani na kuwaacha wengine.''
Alisema marafiki wake walimshangaa sana hasa kwa pesa alizoweza kupata kwa kuuza maziwa yake wakisema ni njia rahisi sana kujipatia pesa na kwamba wanatafakari kufanya hivyo na wao

Related Posts:

  • Papa Francis aweka mambo hadharani Papa Francis jana alikukutana kwa faragha na kundi dogo la waathiriwa wa unyanyasaji wa kimapenzi waliotendewa na mapadri wa kikatoliki. Ni mara ya kwanza kukutana na waathiriwa hao tangu achaguliwe … Read More
  • Watu 50 wakamatwa wanaoshukiwa katika milipuko Kenya.   Naibu Rais wa Kenya Wiliam Ruto amesema washukiwa 50 wamekamatwa kuhusiana na machafuko yaliyotokea siku chache zilizopita katika eneo la pwani ya Kenya. Serikali imeahidi kuwasaka wote waliohusika na mashamb… Read More
  • Mamia wateketea na Ebola Afrika Magharibi.   Maafisa wa afya wa Afrika Magharibi wanasema watu 25 zaidi wamekufa kutokana na maradhi ya Ebola tangu Julai 3, na kusababisha idadi ya waliokufa hadi sasa kufikia 518. Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema … Read More
  • Obama aomba msaada wa dharura Rais Obama ameielezea hali ya uhamiaji kuwa mzozo wa kibinaadamu Rais Obama anaomba dola bilioni 3.7 za msaada wa dharura kutoka bunge la Marekani kusaidia kukabiliana na ongezeko la watoto waliohama peke yao kutok… Read More
  • 20 wauawa katika shambulio la anga, Gaza Mashambulio ya anga yaliyofanywa na Israel yamewaua zaidi ya watu 20 katika eneo la Gaza, wakiwemo raia. mashambulio hayo yanatazamiwa kuwa mwanzo tu wa oparesheni kubwa inayopangwa kufanywa na Is… Read More

0 comments:

Post a Comment