Facebook

Wednesday 3 December 2014

Mashine inayofikiri zaidi ya uwezo wa binadamu yahatarisha maisha.

Profesa Stephen Hawking, mmoja wa
wanasayansi mahiri nchini Uingereza,
amesema juhudi za kutengeneza mashine
inayofikiria inatishia uwepo wa binadamu.

Amesema
"Kutengenezwa kwa mashine
yenye uwezo wa kufikiria inaashiria
maangamizi ya binadamu."
Onyo la Profesa Hawking limekuja kutokana na
kuimarishwa kwa teknolojia anayotumia katika
mawasiliano, ambayo inahusisha msingi wa
Akili Bandia(Artificial Intelligence, AI).
Lakini wengine hawana upinzani sana na
matarajio ya teknolojia hiyo ya AI.
Mwanasayansi huyo wa nadharia ya fizikia,
ambaye anaumwa ugonjwa wa mishipa ya
fahamu (ALS), anatumia mfumo mpya
uliotengenezwa na kampuni ya Intel
kuzungumza.

Wataalam wa mashine za kujifunza kutoka
kampuni ya Uingereza ya Swiftkey pia
walihusika katika kuunda mashine hiyo.
Teknolojia yao, tayari inatumika kama mfumo
wa smartphone, unajifunza namna Profesa
Hawking anavyofikiria na kupendekeza maneno
ambayo huenda angetaka kuyatumia baadaye.

Profesa Hawking amesema miundo duni ya
akili bandia (AI) ambayo imeboreshwa mpaka
sasa imethibitisha kuwa na manufaa sana,
lakini ana wasiwasi wa madhara yanayotokana
na kuunda kitu chenye uwezo sawa na
binadamu au kupita. "Mashine hiyo inaweza
kujiwasha na kujizima na kujibadili yenyewe
katika kiwango kisichomithilika," amesema.

Cleverbot ni kifaa(software) ambacho
kimeundwa kuwasiliana kama binadamu
anavyofanya "binadamu ambao wana ukomo
wa kufikiri kutokana na mabadiliko ya taratibu
ya kibaolojia, hawawezi kushindana na mashine
hii, na watapitwa kwa mbali."

0 comments:

Post a Comment