Facebook

Thursday, 3 July 2014

Ajali ya ndege yawaua watu wanne Kenya

Ajali ya ndege Nairobi
Shughuli za uokozi zikiendelea baada ya ndege ya mizigo kuanguka jijini Nairobi
Watu wanne akiwemo Rubani wa ndege moja ya mizigo, wamefariki dunia baada ya ndege walimokuwa kuanguka mapema leo asubuhi katika mtaa wa Embakasi jijini Nairobi.
Kwa mjibu wa shirika la msalaba mwekundu nchini Kenya, ndege hiyo ilianguka dakika chache tu baada ya kuruka kutoka katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta.
Ndege hiyo ya mizigo ilikuwa imebeba shehena ya Miraa ama Mairungi kuelekea Mogadishu nchini Somalia.
Uchunguzi umeonyesha kuwa ndege hiyo huenda iligonga mlingoti wa stima karibu na mtaa wa Embakasi, mjini Nairobi na kuanguka.

Related Posts:

  • HATIMAYE KIONGOZI WA AL SHABAB AUAWA Aliyekua kiongozi mkuu wa Alshabab Ahmed Abdi Godane ameripotiwa kuuawa!! Habari kutoka katika idara kuu ya ulinzi ya marekani PENTAGONI imesema kua kuuawa kwa kiongozi huyo mwanzilishi wa kikundi ambacho kimekua mwiba mkali… Read More
  • KESI YA KENYATTA YAPIGWA KALENDAWaendesha mashtaka katika Mahakama ya Kimataifa ya ICC iliyopo The Hague wameomba kesi ya Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta kuahirishwa tena. Bwana Kenyatta anashtakiwa kwa makosa dhidi ya ubinaadam, lakini upande wa mashtaka umes… Read More
  • Damu ya waliopona Ebola kutibu Wagojnwa wengine. Shirika la afya duniani WHO limesema kuwa damu ya watu ambao wamepona ugonjwa wa Ebola inaweza kutumiwa kuwatibu wagonjwa wengine. Katika mkutano mjini Geneva, wataalam wa shirika hilo walikubaliana kwamba hii itakuwa njia ya… Read More
  • Boko Haram wazuia watu kuzika maiti Wapiganaji wa Boko Haram wamesababisha maafa Kaskazini ya Nigeria ngome yao ya vita Taarifa za kutisha zimeibuka kutoka mjini Bama moja… Read More
  • Mafuriko yaua nchini India Watu kadhaa wanahofiwa kufa baada ya basi walilokuwa wakisafiria kuchukuliwa na maji katika jimbo la Kashmir nchini India. Basi hilo … Read More

0 comments:

Post a Comment